Kaka Michuzi,

Kwa masikitiko makubwa sana napenda kuwaeleza wana blog hii kitu ambacho kilitutokea mimi na wenzangu huko Zanzibar.Wakati wa likizo ya pasaka tuliamua kwenda Zanzibar kupumzika tukiwa kama kundi la watu 5 hivi kutoka Tanzania bara.Kufika Zanzibar tukaelekea Shamba ambako kuna hotel nyingi na tukaamua kwenda kuulizia accomodation kwenye hotel moja inayoitwa Baobao beach bungalows.

Kufika getini tukakuta walinzi wamasai.Cha kushangaza kwanza hao walinzi wakaja kwenye gari letu na kuangalia ndani kuna akina nani,walipotuona wakarudi ndani wakafunga geti halafu mmoja akaja akatuuliza tuna shida gani.Baada ya kumwambia tunauliza accomodation akajibu hapa hawalali watu weusi,hapa ni wazungu tu tena kwa majigambo.

Nilipata hasira sana nikatamani hata kufanya fujo.Huyo mmasai mwenyewe ni mweusi sana kupita mimi.Tukamwabia tunataka kuongea na meneja,hawakumwita tukapiga honi sana hapo getini hamna aliekuja zaidi ya hao masai.Siku iliofata tukaamua kwenda hapo kula chakula cha mchana,hata kabla hatujaingia tukafukuzwa na walinzi wa kimasai eti sisi watu weusi hapo ni wazungu tu.

Wadau nataka kujua katika hii nchi yetu kuna hotel za kulala wazungu tu,na kama zipo ni zipi tuzijue ili siku nyingine tusije kusanya vi cent vyetu twende vacation tufukuzwe kama tulivyofanyia hapo Baobao beach bungalows.

Mimi
Mtalii wa Ndani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 01, 2012

    Naomba viongozi wanaohusika wachunguze tuhuma hizi haraka iwezekanavyo. Ubaguzi wa rangi hasa kwa wananchi ni aibu Tanzania, na kama unaachiwa kuendelea huku viongozi wanaliona, ni mojawapo ya sababu kubwa inayowafanya wanachi kuona kwamba serikali haiwajali wao bali inawajali wawekezaji.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 01, 2012

    hao wamasai walikua washenzi.. Mungeenda kutoa ripori, hoteli ingefungiwa hiyo..

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 01, 2012

    mie nimeshawahi kwenda Nungwi na sikuruhusiwa hata kuingia katika hotel kama tatu hivi. nilipouliza nikaambiwa sio kwa ajili ya wazungu. hotel hizo ni kwa ajili ya waitaliano tu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 01, 2012

    Kuna mchezo mchafu huko mngekubaliwa kufanyiwa?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 01, 2012

    tunashukuru mdau kwa kuliweka hili katika mwanga kwani wengine hatujui kama mambo haya yanaendelea hadi leo.
    kwamba hata ukiwa na fedha bado unabaguliwa rangi tena ndani ya nchi yako?

    nadhani hao wamasai wamepewa amri hiyo kutoruhusu watu weusi kuingia. suala hili linatakiwa liripotiwe kwenye mamlaka husika mapema na pia hao watu wachukuliwe hatua kali kwani ubaguzi huoo ukikua utaendelea hadi kwenye maduka, majumba ya kupangisha, malls, supermarket, mitaa, na hata barabara, mwishowe tutaingia kwenye machafuko kwani uvumilivu utakosekana kwa wenye nchi hata kama ni masikini.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 01, 2012

    nilifikiri wazenji ndo wamewabagua kumbe wabara wenzenu.

    mnabaguana wenyewe kwa wenyewe halafu mnataka kulaumu watu wengine.

    na mlinzi angekuwa mzenji basi uislamu ndo ingekuwa kosa na huku safari ilikuwa ya pasaka ndo usiseme.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 01, 2012

    Zanzibar ina damu ya ubaguzi. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuruhusu ujinga kama huo ndicho kinachosababisha hata Wanzanzibar kuwabagua Wakristo na Wabara. Hiyo dhambi ya ubaguzi itatafuna hivyo visiwa kama serikali haitachukua hatua madhubuti.
    MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 01, 2012

    Ukoloni unarudi tena Tanzania.Wanataka watufanye manamba hawa wazungu,na hawa wamasai nani kawaambia hapo ni kwa ajiri ya wazungu tu inaonekana meneja anahusika.Ya marekani yanakuja Tanzania.Muumba akipenda bado siku chache uhuru kamili utafika.Kila siku nawaelezaga rafiki zangu,Tanzania bado hatujawa na Uhuru kamili.Hata bendera yetu inapepea kwa masaa kumi na mbili,TAFAKARINI WATANZANIA.Michuzi naomba uiweke hii,manake inaonyesha COMMENTS nyingi zikitumwa kwako huziweki sijui na wewe ni mmoja wapo kati ya hao wanaosimamia ukoloni wa kisasa.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 01, 2012

    Ukoloni unarudi tena Tanzania.Wanataka watufanye manamba hawa wazungu,na hawa wamasai nani kawaambia hapo ni kwa ajiri ya wazungu tu inaonekana meneja anahusika.Ya marekani yanakuja Tanzania.Muumba akipenda bado siku chache uhuru kamili utafika.Kila siku nawaelezaga rafiki zangu,Tanzania bado hatujawa na Uhuru kamili.Hata bendera yetu inapepea kwa masaa kumi na mbili,TAFAKARINI WATANZANIA.Michuzi naomba uiweke hii,manake inaonyesha COMMENTS nyingi zikitumwa kwako huziweki sijui na wewe ni mmoja wapo kati ya hao wanaosimamia ukoloni wa kisasa.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 01, 2012

    Ushamba tu unawasumbua....au labda kuna kitu wanaficha humo ndani hebu wachunguzwe!

    ReplyDelete
  11. something need to be done here, we have been hearing these stories for long time now but no one even say something from government officials.

    Governement of Zanzibar please, this is small issue for you to handle, if we allow this to continue one day, Citizen will burn these hotels, mark my word i say one day!!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 01, 2012

    Nyie mnasema hotel, beach za huko wenyeji wenyewe hararuhusiwi kuvua, kupita njia, wala kwenda kuenjoy beach zao. Hiyo nchi tunayoigombea tunataka uvunjike Muungano, mimi nahisi ni shinikizo kutoka nje. Ndege za watalii zinatoka Europe (Italy hasa hasa) moja kwa moja mpaka Zanzibar, sana sana wanapata ile airport charge pesa zote zinawekwa kwenye Account Europe. wao wanakuja wao tu na viroba vyao. Huo utalii unaosemwa kwamba ni kitega Uchumi cha Zanzibar ni kiini macho cha hawa mafisadi wa kizungu au kuna watu wanashirikiana.

    Kuna kipindi nilitumwa kutafuta vyumba Mafia katika Mafia Lodge. Nilizua kasheshe, maana Booking unafanya na mtu yuko Europe, tena unambiwa ni fully booked, baadae wamerealize ni Serikali ndio imeomba hizo bookings bwana tulikuwa harrased hapo. Mafia lodge haina hadhi ni mbaya. Hawa wana ajenda za siri. This is neo-colonialism fully entrenched.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 01, 2012

    Ni kweli kabisa asemacho huyu mdau, kuna hotel haziruhusu weusi kabisa.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 01, 2012

    mie nilienda mwezi november 2011 kule Nungwi, nikajaribu kupata dinner katika hotel kama tatu tofautil nilikatazwa hata kuingia, nikaambiwa hizo hotel ni kwa ajili ya waitaliano tu. hata wazungu wengine hawaruhusiwi kuingia sio waafrika pekee.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 01, 2012

    Nijuavyo hizi hotel za kitalii nyingi hasa za Arusha nikweli ukienda unarudishwa, lakini sikwasababu ni mweusi, no!. You must book on line so if you are at the gate you show them your booking. Ndiyo utalii ulivyo hakuna cha sura, masai huyo msamehe bure. Mimi nisafiripo nafanya booking on line na jiwahi pata shida kwenye gate na hawo wamasai.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 01, 2012

    chunguzeni jambo hili na kama ni kweli watu wawajibike because hawa wataliano wanaleta zao za kuleta za kigaidi kila wanapopata kustawi na kujitawala.

    inasikitisha sana lakin wachunguzeni sana ndo maana wanapapenda zanzibar
    na ndo maana tunataka kutoa ufisadi huu tupate nchi yetu

    mdau switzerland

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 01, 2012

    ubaguzi wa wataliano unajulikana, nashangaa wazenji hawaoni hayo, wanaona wabara tu na makanisa? wazenj wana info zote, ngoja tuone kama wataandika sana kama walivyoandika hoja kwenye tukio la wale wenye uamsho

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 01, 2012

    Watu wa utalii wachunguze hili na watujulishe hatua iliyochukuliwa.

    Lakini mbona umechelewa, tangu pasaka mpaka leo?

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 01, 2012

    Ndio maana sishangai, haya maasi yanayoendelea, madawa ya kulevya kila kona.

    Serikali iliyoko madarakani, wakati sasa umefika wa kuamka kutoka usingizi mnono na ianze kufanya kazi sasa. Upinzani umeshika hatamu sasa kwa kuona umkiyapuuzia mambo haya.

    Hivi kwa nini ni Wazungu tu, ina maana kuna biashara fulani zinazoendelea wanatuogopa watanzania maana tupo tunaojua lugha yao ndio maana hawataki kuchangamana. Lakini swala la msingi kabisa kwanini watuchukie na kutubagua sisi weusi hali wako kwenye nchi yetu. Tumechoshwa na hali hii kama serikali haitachukua hatua basi sisi wananchi tutatoa suluhisho.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 01, 2012

    HALAFU WAZANZIBARI WAKIANDAMANA MNAJIFANYA WABARA HAMUELEWI. WASIDIENI WAZANZIBARI WENZETU WANAOANDAMANA, KWA SABABU VIONGOZI WAMELALA.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 01, 2012

    poleni sana wakuu kwa yaliyowapata.Tatizo liko kwa serikali na waendesha hotel kwani wameshindwa kuwaelimisha wananchi/wafanyakazi ili kuwaondolea hiyo imani kuwa hotel tulizonazo hapa nchini ni kwa ajili ya kila mtu awe mzungu au mweusi.Nashawishika kuamini kuwa nyie ndio mlikuwa watalii wa kwanza kwenda pale tangu hao wamasai waajiriwe pale na huenda mmiliki wa hotel kawafundisha walinzi wake kuwa wateja hapa ni wazungu tu.Tanzani bado tuko nyuma sana ktk sekta zote,siwezi hata kuendelea..................agrrrrrrrrrrrrrrrrr

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 01, 2012

    poleni sana wakuu kwa yaliyowapata.Tatizo liko kwa serikali na waendesha hotel kwani wameshindwa kuwaelimisha wananchi/wafanyakazi ili kuwaondolea hiyo imani kuwa hotel tulizonazo hapa nchini ni kwa ajili ya kila mtu awe mzungu au mweusi.Nashawishika kuamini kuwa nyie ndio mlikuwa watalii wa kwanza kwenda pale tangu hao wamasai waajiriwe pale na huenda mmiliki wa hotel kawafundisha walinzi wake kuwa wateja hapa ni wazungu tu.Tanzani bado tuko nyuma sana ktk sekta zote,siwezi hata kuendelea..................agrrrrrrrrrrrrrrrrr

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 01, 2012

    Aibu du!

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 01, 2012

    Mimi ni Mzanzibari kwanza hili lisihusishwe na fujo za juzi,Pili ni kweli kabisa mimi naishi marekani miaka mingi sana

    ,nilipokwenda Zanzibar mwaka 2001 tulikwenda Day out sikumbuki wapi lakini ni shamba sehemu za watalii,nilikuwa nikirikodi rikodi fukwe na ndugu zangu cha kushangaza Wamasai wakaja kunikamata tukashindana nao wakaita Polisi- tukachukuliwa hadi chumba cha upelelezi wakasema ati wataniweka ndani siruhusiwi kuenda sehemu za watalii-nikawambia nami pia ni mtalii na nimekuja kwa ndugu zangu tu hapa wakanikatalia sana

    na kuniambia kuwa watalii wanaibiwa na vile vile recently hoteli zimechomwa moto,yaani wamenifananisha mimi sawa na wahalifu,wakataka nitoe passpoet nikawa sina ,bahati nzuri tulikuwa na Mjomba wa rais wa Zanzibar wakati huo ni Salmin.Katika kuandika statement wakashtuka mkuu wao akasema si hatukutaka kumuweka ndani ila kumfahamisha tu mimi na anapotoka Salmin ni huko huko hatukosani.

    pia akatokezea mwenyeji wangu akawashambulia sana na kuwauliza bahari ni mali ya nani kwani? hata kama hoteli ni ya watalii akatokanana nao sana,lakini wakalazimisha tufute casset tulorikodi.

    kwakuwa elimu ndogo tukafanya tumefuta kumbe zogo lote tunalo.Hiyo ndio hali ya Zanzibar Kumalizia walioko mahotelini lakini ni Watanzania bara mkumbuke.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 01, 2012

    Tatizo ni kuwa na Watawala wanao kumbatia wawekezaji hasa Wataliano,wamasai hao wanatii Amri waliyopewa na Tajiri yao.Chamaana ni kuwataka Watawala watueleze wamesha uza nchi hii tujuwe la kufanya.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 01, 2012

    Wamasai hawana makosa katika hili na wala hawatakiwi kulaumiwa. Wao wamefanya walichoamriwa na uongozi wa hoteli. Ni kweli kuwa hoteli nyingi sana kule zinamahusiano makubwa na wataliano, hivyo wamasai kule wanajua kitaliano kupita kimasai na kiswahili, wengine wameoa wataliano.

    Kibanga Msese

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 01, 2012

    naomba niwasaidie ; tatizo ni uelewa wa hao watu wa mapokezi mleta mada anaonekana sijui ni jazba ama ubaguzi au ni usenzi kaamua kutumia kabila...
    ni hivi kumetokea matukio mengi ya wageni hasa kutoka nchi za nje kuibiwa mali zao wawapo hotelini;ama hoteli yenyewe kuibiwa , watu wanapanga hotel moja na hao wageni usiku wanawasafisha alfajir wana'check out , msala ni kwa mwenye hotel na watumishi wake ... sasa inaelekea maelekezo waliopewa ndugu zetu wa mlangoni wanashindwa kuyasilisha vyema si mnajua kuwa fani ya uhotelia nchi yetu bado la msingi ni kuingia kwenye blog ya hiyo hotel na kuacha coments zako nzdhani watazifanyia kazi insh'allah

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 01, 2012

    Mtu unategemea kuwa kubaguliwa kwenye nchi za wazungu lakin hadi nchini kwako? halafu Serikali na wananchi wanatuambia tuliokuwa overseas "mkataa kwao mtumwa". Wakati huku kitendo kama hicho ungewa-sue kuanzia hotel hadi mmiliki. Ndio Tanzania yetu hiyo...

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 01, 2012

    Halafu waziri wa Utalii na Maliasili anapoadabishwa anasema ameonewa!!

    ReplyDelete
  30. Nitaufikisha ujumbe huu kwa viongozi wa Hotel wahusika leo maana kitendo hiki hakivumiliki hata kidogo,katika nchi yetu wenyewe na bado tunanyanyasana,siku nyingine mnaokuja huku ikitokea jambo kama hilo basi toeni taarifa hata Polisi maana kuwakataa ntie ilikuwa ni tusi tosha na ni udhalilishaji uliovuka mipaka na haivumiliki.
    Poleni sana ila mkumbuke kuwa hawa wamasai ukiacha kutosoma maisha yao hutegemea wazungu wanawake wawape maisha kitu ambacho wakiona waafrika wenzao wanaona hawatapata ngekewa za vibibi vya kizungu.

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 01, 2012

    Wizara ya utalii ituwekee majibu hapa hakuna swala la kubook ukiwa europe mimi niko europe ninakwenda hotel ninapata huduma reception na pia ninaweza kubook online na huyo mtanzania ambae hana creditcard ya europe akibook online afanye nini mimi ninachukia viongozi watanzania hawakusoma wala hawajui wanachokiongoza na pia hawasomi nchi nyingine zinaongozwa vipi sipendi vita lakini kila nikifikiria viongozi wajinga hawa wataondoka vipi tanzania?

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 01, 2012

    YOU: "Nijuavyo hizi hotel za kitalii nyingi hasa za Arusha nikweli ukienda unarudishwa, lakini sikwasababu ni mweusi, no!. You must book on line so if you are at the gate you show them your booking. Ndiyo utalii ulivyo hakuna cha sura, masai huyo msamehe bure. Mimi nisafiripo nafanya booking on line na jiwahi pata shida kwenye gate na hawo wamasai."
    ME: Sasa si waseme kuwa booking unafanya online na sio hotel ni ya watalii tu...Na watanzania tuache kufanya hili jambo la Zanzibar na sio Bara, tulikiwa wote watanzania hili suala ni letu wote.
    Na kuna mdau amesema kama America, hell no!! America unahisi umebaguliwa lakini utakuwa na wakati mgumu ku-prove hayo yalikuwa mambo ya 1950's. America ya leo hakuna anayeweza kukwambia watalii tu na weusi hawaruhusiwi. By the way, ukiwa mtalii mweusi inakuwaje?

    ReplyDelete
  33. AnonymousJune 01, 2012

    BAOBAB BEACH BUNGALOWS:

    Hatutaki ujinga katika ardhi ya Tanzania iliyo huru!

    HAIWEZEKANI UJINGA KAMA HUU KUJIRI KTK TANZANIA ILIYO HURU!!!

    LAZIMA HAWA JAMAA WAPEWE MASAA 24 WAONDOKE NCHINI NA HAO NDUGU ZETU WAMASAI INATAKIWA WAFUNGWE ILI IWE FUNDISHO KWA WENGINE KAMA WATAPEWA AJIRA YA KITUMWA KAMA HIYO WAKATAE NA WATOE TAARIFA HARAKA SERIKALINI!!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...