Ndugu wapendwa,
Tunatafuta ndugu wa Sadock Mgamba ambae anaumwa sana huko Dodoma. Wote tunaomfahamu Sadock tunajuana kama rafiki yetu wa karibu, lakini kwa bahati mbaya hakuna anayemjua ndugu yake wa karibu.
Kwa sasa yeye ni mgonjwa kiasi cha kushindwa kuwataja ndugu zake.
Tunaomba sana kwa yeyote anayefahamu ndugu yake aliko au anajua mtu yoyote wa karibu tunaomba awasiliane na Mchungaji Fue wa Tumaini University anayemhudumia mgonjwa wetu katika numba ya simu 0754823970 . Information za Sadock ni kama ifuatavyo:
1. Birth date: 01/07/1969
2. Place: Mwanga Kilimanjaro
3. Primary school: Mfinga iliyoko Ugweno/Usangi
4. Secondary school: Shigatini
5. Next of kin: Godfrey Mghamba (brother) Box 1103 Arusha
Rahib Mchomvu (brother) Box 10476 Dar
Pia Sadock amesoma ACCA pale Salford Greater Manchester UK na alifundisha Tumaini Mwaka 2007 na 2008.
Kila mtu asomae ujumbe huu tunaomba sana amjulishe mwenzake ili tufanikishe kazi ya kumtafutia rafiki yetu Sadock Mghamba ndugu zake
Kwa kuwa alisoma shule ya msingi Mfinga inafikiriwa kuwa huko ndiko nyumbani kwao ambako ni Ugweno au Usangi.
Tumwombee Sadock Apone Haraka
Tafadhari sana tuma kwa marafiki zako ili tufanikishe zoezi hili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2012

    Mungu amjalie afya apone haraka na ndugu wapatikane kwani nayo itakua ni faraja kwa mgonjwa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2012

    Jamani pole sana kaka Sadock. Kumbukumbu yangu ni kama vile alisoma ADCA Mzumbe akamaliza 1994

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 08, 2012

    namjua mghamba mmoja lakini wao wanatoka kijiji cha muhezi namuuliza amuulize mzee wake kama ndie wata respond kwenye contacts hapo juu

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 08, 2012

    SASA JAMANI WENZETU WASOMI YAANI MNAISHI HATA BILA MAWASILIANO NA NDUGU ZENU KWELI MPAKA MATATIZO NDIO MNAANZA KUTAFUTA NDUGU?

    HANA HATA GIRL FRIEND HUYO KIJANA AMBAYE LABDA ANAWEZA HATA KUWA ANAMFAHAMU RAFIKI YAKE HATA MMOJA.

    MUNGU AMPE AFYA NZURI LAKINI MOLA AKIMJALIA LAZIMA AENDE AKATAFUTE NDUGU NA AKAANGUKIE MAKABURI YA WAZEE KAMA WASHAKUWA MAREHEMU. NI MUHIMU KATIKA MAISHA YETU.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 08, 2012

    Wapare wekeni kando ubahili wenu sasa thi mnajua 'charity begins at.....'

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 08, 2012

    Huyo bila kabisa shaka ametoka mfinga-ugweno, Mwanga. Mh Maghembe (Mb)wa Mwanga, anaweza kutusaidia kwani ni maeneo hayo hayo ametoka na kufahamu familia yake itakuwa rahisi sana.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 08, 2012

    Kazaliwa 69 ina maana alikuwa hana mke; au na mke hakujuhi ukweni. Jamani tuwe karibu na familia zetu maana maisha haya hatujuhi ya kesho; ndugu ni ndugu hawawezi kututupa.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 08, 2012

    AHSANTE NISHAWAPATA NDUGU ZAKE NIMEWAPA NAMBA YA HUYO MCHUNGAJI NI WA KIJIJINI KWETU KABISA, JAPO SIMFAHAMU

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 08, 2012

    Pole sana Ndugu yangu Sadock getwell soon jembe langu.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 08, 2012

    Ndg. Sadock Mgamba pole sana na Mwenyezi Mungu atakudhamini zaidi ukapata nafuu na kupona kabisa!

    Sasa Mchungaji Fue ungetoa namba ya M-Pesa ili angalau Wadau na sisi tujikakamue kwa kutoa chochote kwa ajili ya huduma kwa mgonjwa!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 08, 2012

    mtoa tangazo umejichanganya..umetupa majina mawili ya kaka wa mgonjwa, si muwatafute hao. Je kusema hawezi kuwataja ndugu, wakati wewe umewataja unamaanisha nini? ndugu ni hao, japo ni p.o. box address, mkiweka tangazo katika Luninga, hao makaka wawili watajitokeza na kutoa taarifa kwa ndugu wengine, wazazizi nk..

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 08, 2012

    Sad. So sad. I find a profile in facebook with 19 friends. Does it means none of them cares?
    Namwombea afya na uzima.
    Blackmpingo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...