RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein ametanabaisha na kusisitiza juu ya umakini mkubwa unaohitajika katika kuandaa, kusimamia na kufuatilia Mikataba ya Mafuta na Gesi ili kuepuka ubabaishaji kwani rasilimali hizo ni za Wazanzibari wote. 
Alhaj Dk. Shein aliyasema hayo leo katika hotuba yake aliyoitoa katika Baraza la Idd El Fitri lililofanyika huko katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi, Kikwajuni Mjini Zanzibar. 
Alisisitiza kuwa mikataba ya Mafuta na Gesi Asilia isitoe mwanya wa kuwanufaisha watu wachache na makampuni yao kwa njia za kijanja, dhulma na mambo ya ubabaishaji na kutaka kujifunza kwa waliotangulia katika biashara ya aina hiyo. 
Katika hotuba yake, Dk. Shein alisema kuwa baada ya kukamilika kwa kazi ya kutunga Sheria ya Mafuta na Gesi Asilia, kuanzisha Mamlaka ya Kusimamia na kuratibu shughuli za Mafuta na Gesi na kuanzisha Kampuni ya Mafuta, hatua muhimu inayofuatana ni kuandaa Mikataba ya Mafuta na Gesi Asilia.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Dini na Mashekhe wa Dini ya Kiislamu waliofika  Ikulu Mjini Unguja   leo kumtakia  Rais Sikukuu njema baada ya kumalizika kwa  Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein  pampja na Viongozi mbali mbali wa Dini na Mashekhe wa Dini ya Kiislamu waliofika  Ikulu Mjini Unguja   leo kumtakia  Rais Sikukuu njema baada ya kumalizika kwa  Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,wakiitikia Dua Iliyoombwa na Mufti Mkuu wa Zanzibae Sheikh Saleh Omar Kabi
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)alipokuwa akitoa Sikukuu kwa Mzee Juma Kesi (kulia) alipojumuika na Wazee mbali mbali waliofika katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja  kupokea mkono Eid el Fitri katika kusherehekea Sikukuu ya  Eid el Fitri iliyoanza leo baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) aliopokuwa akitoa hutuba yake kwa Wananchi na Waislamu mbali mbali katika Sherehe za Baraza la Eid el fitri lililofanyika   katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi, Kikwajuni Mjini Unguja katika   kusherehekea Sikukuu ya  Eid el Fitri iliyoanza leo baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan
 Baadhi ya Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi na Wananchi mbali mbali wakisikiliza Hutuba ya sherehe za  Baraza la Eid el fitri iliyosomwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani )  katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi, Kikwajuni Mjini Unguja katika   kusherehekea Sikukuu ya  Eid el Fitri iliyoanza leo baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...