KUKAMILIKA kwa mchakato wa uaandaaji wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutasaidia kuweka misingi imara na kuondoa changamoto zilizopo katika Katiba ya sasa, hivyo kukomesha ufisadi na kuinua uchumi wa Tanzania.

Aidha, kukamilika huko kwa Katiba Mpya kutaakisi jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.

Hayo yalisemwa hivi karibuni na Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Blaston Gaville, ambaye alimtaka Rais Magufuli kuumalizia mchakato wa kuandikwa kwa Katiba Mpya, kwani alisema mbali ya kuakisi kasi yake anayoifanya ya kukuza uchumi pia kutasaidia kuhimiza uwajibikaji.

“Wakristo na Watanzania kwa ujumla tuna imani kubwa na Serikali ya Awamu ya Tano na ni matarajio yetu kwamba mchakato wa kuandika Katiba utamalizwa kama lengo lilivyokuwa,” alisema. 

Askofu Gaville amesimikwa ili kuchukua nafasi ya Askofu Dkt. Owdenburg Mdegella ambaye amestaafu.Alisema wanatiwa moyo na jitihada zinazoendelea kufanywa na Dkt. Magufuli katika kufufua uchumi na kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumika kwa manufaa ya Watanzania wote. 
Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Blaston Gaville (kushoto).
Askofu Blaston Gaville wakati akiwekwa wakfu kuongoza Dayosisi ya Iringa ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...