Ecobank yaja na suluhisho la kufanya malipo salama kwa njia mtandao kupitia MASTERPASS na MVISA . 

Ecobank katika kuendeleza dhamira yake ya kutoa huduma bora na kuwa suluhisho kwenye sekta ya biashara ya huduma za kibenki hapa nchini leo imezindua applikesheni ya simu za mkononi itakayojulikana kama Ecobank Mobile App – MASTERPASS NA MVISA ili kusaidia wafanyabiashara na watoa huduma mbalimbali kufanya Malipo kwa njia rahisi na kwa usalama zaidi mahali popote.

Mtanzania yeyote ataweza kutumia teknolojia hii ya mpya ya MASTERPASS QR na MVISA kulipia gharama mbali mbali kwa kutumia simu zao za mkononi kwa kupitisha Quick Response (QR) kwa wauzaji mbalimbali wa bidhaa au watoa huduma ndani na nje ya nchi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania Bi, Mwanahiba Mzee alisema “applikesheni ya Ecobank Mobile App ilizinduliwa Februari mwaka huu lakini kwa sasa imeboreshwa zaidi ili wateja wa Ecobank na wale wasio wateja wa bank hii waweze kutumia applikesheni hii duniani kote”.

‘Applikesheni ya Ecobank Mobile App ni njia rahisi ya kujipatia huduma za kibenki ndani ya nchi 33 ambazo Benki yetu inafanya biashara lakini pia unaweza kuitumia ukiwa kokote duniani. Wateja wanaweza kupakua applikesheni Ecobank Mobile App na papo hapo kujifungulia akaunti ya Ecobank kwa njia ya mtandao na kuanza kupata huduma za kibenki kama vile kufanya malipo au kuhamisha fedha bila kutembelea tawi lolote la Benki”, alisema Bi Mzee.

“Tunayo furaha kwamba applikesheni yetu ni sulushisho la huduma za haraka za kibenki kupitia mtandao wa simu za mkononi na bado inaendea kuboreshwa zaidi na zaidi na sasa tunatumia teknolojia ya Masterpass QR na Mvisa kwa kufanya malipo mbali mbali, aliongeza. 
  Mkurugenzi  Mtendaji wa Benki ,Ecobank Tanzania, Mwanaiba Mzee, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa Uzinduzi  huduma ya Malipo kwa njia ya Mtandao, inayayojulikana kama MasterPass na MVISA .Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki  hiyo, Respige  Kimati  na Mkuu wa Kitengo cha wateja wa Reja reja, Ndabu Sware (kushoto).
 Mkuu wa Kitengo cha wateja wa Reja Reja wa Ecobank Ndabu Lilian Sware (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa Uzinduzi  huduma ya Malipo kwa njia ya Mtandao, inayayojulikana kama MasterPass na MVISA. Kati kati Mkurugenzi  Mtendaji wa Benki hiyo Mwanaiba Mzee na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki  hiyo, Respige  Kimati.
Baadhi ya wafanyakazi wa Ecobank Tanzania wakifuatilia kwa umakini wa Uzinduzi  wa huduma ya Malipo kwa njia ya Mtandao, inayayojulikana kama MasterPass na MVISA. Ecobank Tanzania inakuwa Benki ya kwanza hapa Tanzania kuzindua huduma ya Mobile App ambayo inakuwa ni suluhisho kwa huduma za kifedha.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...