Tangu umetuacha tumetafakari mengi tukidhani umesafiri utarudi lakini kumbe haikuwa hivyo. Kuwa kwako mbali na familia kumetufanya kujifunza mengi kuhusu maisha na kutafakari muda ambao tulikuwa pamoja katika maisha ya hapa duniani wakati wa furaha na uchungu.

 Unakumbukwa na mke wako Rose na watoto wako Martina, Grace, Gideon, Gonsalver na Gibson. Umetimiza mwaka sasa tangu umetuacha; pengo lako ni kubwa katika kila kona ya maisha na hata katika Tasnia ya Habari uliyoitumikia katika muda mwingi wa maisha yako kwa kutuonyesha kwa vitendo maana ya kuipenda na kuithamini kazi katika maisha. 

Tumekosa simulizi za kusisimua za Utalii wa Ndani, ulichimba na kuchimbua mengi ambayo kama si kwa jitihada zako binafsi tusingeyajua kamwe… tumebaki na msemo wako maarufu “Falsafa ya Ufagio ni Unyenyekevu”. Faraja yetu ni Mungu aliye Baba wa Yatima na mume wa Wajane (Kutoka 22:22-24). Tunaamini katika Ufufuo na Uzima na siku moja tutafurahi nawe mbinguni (Yohana 11:25-26). 

Mungu akupe pumziko la Milele, upumzike kwa Amani - Amina

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...