NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI

MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo amesitisha mkataba na Kampuni ya Mwamkinga Auction Mart and Brokers iliyokuwa ikifanya kazi ya kudhibiti uegeshaji wa magari katika maeneo yasiyo rasmi kwa Hal
mashauri ya Temeke na Kigamboni.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa mapema leo asubuhi Meya Mwita amesema kuwa amefikia uamuzi huo kutokana na kampuni hiyo kufanya kazi kwakutozingatia matakwa ya mkataba na hivyo kuanzisha migogoro isiyo ya lazima baina ya halmashauri ya jiji na Wananchi.

Meya mwita amefafanua kuwa jiji liliingia mkabata na kampuni hiyo Aprili mwaka huu kwa lengo la kufanya kazi hiyo ambapo mkataba huo ulielekeza kufanya kazi kwa weledi mkubwa, kuzingatia sheria, miongozo ,maelekezo, kanuni na taratibu zilizopangiwa bila kusababisha bughudha, uonevu, kero na usumbufu kwa wananchi jambo ambalo halikufanyika.

“ Hii kampuni imekuwa ikilalamikiwa mno na wananchi, inawasumbua, na sisi kuwapa tenda hii sio kwa ajili ya kuwanyanyasa, kuwasumbua ila ni kufanya kazi kwa weledi”Nakuongeza kuwa” tumefuatilia kwa karibu sana utendaji kazi wao, kutokana na malalamiko ambayo yalikuwa yanatolewa na wananchi, tukajiridhisha, kwa ushahidi uliojitosheleza, hawawezi kunyanyasa watu na mimi kama meya wa jiji hili nikawaachia, hili haliwezekani” amesisitiza Meya Mwita.

Hata hivyo ameeleza kuwa kampuni hiyo inapaswa kuondoka mara moja kwenye maeneo iliyopangiwa kufanya kazi hiyo na kuhakikisha kwamba katika kuanzia tarehe ambayo mkataba huo umesitishwa iwe imekabidhi mashine zote za kukusanyia mapato kwa halmashauri zikiwa kwenye hali salama.

Aidha Meya Mwita amesisitiza kuwa hata sita kuzichukulia hatua kampuni nyingine ambazo zimepewa tenda hiyo na kuzionya kuwa iwapo wanatabia hiyo waache mara moja kwani kazi waliyopewa sio ya kusanyanyasa wananchi bali ni kufanya kazi kwa kufuata sheria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...