Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto akiwa katika picha nchini China mara baada ya kuwasili kuiwakilisha Tanzania katika Tamasha la Utalii Duaniani. 
 Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto amewasili nchini China leo katika eneo ambalo litakuwa likionesha utalii ikiwa ameenda huko kwaajili ya kuwakilisha nchi katika tamasha la Utalii Duniani ambalo litafanyika kuanzia Leo Septemba 21,2017.
Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto akiwa na mwenyeji wake katika viwanja ambavyo Tamasha la Utalii linafanyika nchin China.

Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto amewasili nchini China Jumatano hii kwaajili ya kuiwakilisha Tanzania katika Tamasha la Utalii Duaniani. 

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Kitendawili’, aliondoka nchini Tanzania siku ya Jumatatu akiwa ameambatana na kikundi chache cha ngoma kikiwa na jumla ya watu sita pamoja na yeye mwenyewe.
Akiongea na mwandishi wetu akiwa nchini humo baada ya kuwasili katika eneo ambalo litafanyika tamasha hilo, Mpoto amesema Alhamisi hii wataanza kufanya maonyesha hayo katika tamasha hilo ambalo linayakutanisha mataifa mbalimbali duniani.

“Kama nilivyowaambia watanzania wakati naondoka Tanzania, tumekuja China kwaajili ya watanzania, tumekuja kuwawakilisha wao, tunatangaza utalii wa ndani, lugha zetu za makabila zaidi ya 120, lugha yetu hadhimu ya Kiswahili, mbuga zetu za wanyama kwahiyo sisi tutawaambia Tanzania ni nchi ambayo ina kila kitu kama ukiamua kuitembelea,” alisema Mpoto.

Aliongeza,“Tumejiandaa vizuri kufanya kile kitu tulichokipanga, watanzania wananijua mimi ni mtu gani kwenye hizo anga, Kiswahili ni lugha yangu kwahiyo naweza kusema tumejipanga kuuonyesha ulimwengu tuna kitu gani ambacho tumewaletea na bila shaka kila ambaye amekuja katika eneo hili atondoka na meseji ya Tanzania ni sehemu sahihi ya kuitembelea,”

Pia amewataka watanzania kuwaunga mkono wasanii ambao wanafanya jitihada mbalimbali za kuitangaza Tanzania katika nyanja mbalimbali za utalii kwa kuwa utalii ni moja kati vyanzo vizuri vya mapato nchini.

“Uwepo wangu mimi hapa sio kwaajili ya familia yangu, hiki ninachokifanya hapa ni kwaajili ya watanzania, yule mtalii ambaye atakuja Tanzania baada ya kusikia meseji yangu ile pesa anayolipa kwaajili ya kutalii ndio ile ambayo inajenga hospitali na kununua dawa. Kwahiyo mimi ningewataka watanzania kuwa wazalendo kwenye mambo ya msingi ambayo bila shaka yanaleta tija kwaajili ya watanzania wote," alisema Mpoto.
Muimbaji huyo amesema kila mtanzania anaweza kuitangaza nchini yake kwa mazuri hivyo wamewaka watanzania kuwa wazalendo na kudumisha amani iliyopo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...