WADAU katika sekta ujenzi nchini wametakiwa kutumia bidhaa zenye
viwango na ubora unaostahili ili kulinda ukuaji wa sekta hiyo na
kuleta matokea chanya kwa ustawi na maendelea ya taifa na watu wake.
Akizungumza kwenye semina iliyowakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo
wahandisi, makandarasi, wazalishaji, wasambazaji na watumiaji wa nyaya
za umeme jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwango
wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bi. Edna Ndumbaro alisema
bidhaa zinazotumika kwenye masuala ya umeme zinahitaji kuwa na
viwango na ubora unaostahili.
“Badiliko la rangi mpya za nyaya za umeme (New Colour Codes)
limewaleta wadau hawa muhimu kujadiliana kwa pamoja na kuazimia kwa
pamoja namna bora ya utekelezaji wake,” Bi. Ndumbaro alisema.
Alisema rangi mpya ya nyaya ya umeme ilishaazimiwa kama kiwango cha
lazima kufuatwa tangu mwaka 2016 na hivyo ni vyema kwa wadau na
wataalamu wakazingatia kuwa viwango ni jambo muhimu sana likapewa
kipaumbele zaidi.
“Sisi kama TBS tutaendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa viwango na
ubora kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii
ikiwemo tovuti ya shirika,” Bi. Ndumbaro alisema na kuongeza kuwa
washiriki wa semina hiyo watakuwa walimu wazuri.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwango wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bi. Edna Ndumbaro akisisitiza jambo kwenye Semina ya wadau kwenye semina iliyowakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wahandisi, makandarasi, wazalishaji, wasambazaji na watumiaji wa nyaya za umeme jijini Dar es Salaam jana kuhusu matumizi ya Rangi mpya za nyaya za umeme.
Afisa Viwango wa Viwango wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Henry Massawe akiwasilisha mad kwenye Semina ya wadau kwenye semina iliyowakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wahandisi, makandarasi, wazalishaji, wasambazaji na watumiaji wa nyaya za umeme jijini Dar es Salaam jana kuhusu matumizi ya Rangi mpya za nyaya za umeme.
Baadhi ya washiriki wa semina ya wadau kwenye semina iliyowakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wahandisi, makandarasi, wazalishaji, wasambazaji na watumiaji wa nyaya za umeme jijini Dar es Salaam jana kuhusu matumizi ya Rangi mpya za nyaya za umeme semina hiyo imeandaliwa na Shirika Viwango wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...