TAMASHA la ngoma za kitamaduni lililopewa jina la Tulia Traditional Dance Festival, limeanza kwa mbwembwe mjini Tukuyu, mkoani Mbeya jana, likishirikisha vikundi zaidi ya 100 kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini ambapo litafikia tamati kesho.  

Akizungumza tamasha hilo akiwa Tukuyu jana, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson ambaye ndiye mwasisi wake, alisema kuwa anajisikia furaha kuona tukio hilo limepokewa vizuri mno na wakazi wa Tukuyu na mkoani Mbeya, lakini pia na Tanzania kwa ujumla.

“Maandalizi yanaendelea vizuri na mwitikio umekuwa mkubwa mno kuonyesha jinsi Watanzania wanavyothamini tamaduni zao. Matamasha kama haya ni muhimu mno kwani hutoa fursa ya kutangaza utamaduni wetu wa kitanzania na kuwa moja ya kivutio badala ya kutegemea vivutio vya kiutalii vilivyozoeleka kama Mlima Kilimanjaro, mbuga na hifadhi za wanyama na vinginevyo.

“Nawaomba wabunge waandae matamasha kama haya katika maeneo yao ili baadaye washindi watakaopatikana, waweze kushiriki katika tamasha letu hili ili kulifanya kuwa la kitaifa zaidi, hii itasaidia kuwaonyesha vijana wetu wa kizazi cha sasa kufahamu tamaduni zao, kuona mababu zao walikuwa wakifanya nini.

“Kwa serikali, iandae na kuunga mkono matamasha ya utamaduni kama sehemu ya kuenzi utamaduni wetu kwani vijana wengi wamekuwa wakibobea katika tamaduni za kigeni kutokana na kutofahamu tamaduni zao,” alisema.
 Kikundi cha ngoma ya asili ya Sindimba toka mkoa wa Mtwara,Wakicheza ngoma hiyo jana wakati wa mashindano ya ngoma za asili yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania PLC ya”Tulia Traditional dances festival 2017”yanayofanyika kwa siku tatu katika viwanja vya tandale mjini Tukuyu wilaya ya Rungwe mkoa wa Mbeya.
 Wakazi wa Tukuyu wilaya ya Rungwe mkoa wa Mbeya wakifatilia mashindano ya ngoma za asili yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania PLC ya”Tulia Traditional dances festival 2017” yanayofanyika kwa siku tatu katika viwanja vya Tandale mjini humo.
 Majaji wa mashindano ya ngoma za asili yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania PLC ya”Tulia Traditional dances festival 2017” wakifatilia kwa karibu mashindano hayo yanayofanyika kwa siku tatu katika viwanja vya tandale mjini tukuyu wilaya Rungwe mkoani Mbeya.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakimfanyia mahojiano Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Rosalynn Mworia kuhusiana na mashindano hayo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...