Waziri anayeshughlia masuala ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amekutana na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salim Al Ismail na kujadili suala zima la uwekezaji wa viwanda katika Sekta ya Mifugo na Uvuvi.
Katika Mazungumzo hayo Waziri Mpina amemueleza  Waziri huyo wa uwekezaji wa Oman kuwa Tanzania imekuwa ikizalisha nyama kwa kiasi cha tani 36 kwa siku na imekuwa ikifanya biashara kwa kuuza tani za nyama ambazo hazijakatwa katika nchi za falme za kiarabu ikiwemo Oman, na wakati umefika sasa kwa nchi hizi mbili kushirikiana kwa pamoja katika Sekta hii kwa Oman kuwekeza katika Viwanda vya ndani vya nyama kwa kuendeleza viwanda vilivyopo na hata kujenga Viwanda vipya, akitolea mfano ujenzi wa kiwanda cha nyama cha Ruvu ambao umefikia 51% kukamilika.
“Tunataka viwanda vyote vya nyama vya ndani vikidhi mahitaji na kuweza kuuza nyama nje ya nchi”. Alisema Mpina.
Kwa upande wake Waziri Salim Al Ismail alipoelezwa kuhusu viwango na madaraja mbali mbali ya nyama nchini na mmoja wa mtaalam kutoka wizara hiyo, alisema kuwa Oman ipo tayari kuwekeza katika sekta ya viwanda vya nyama na kuisaidia Tanzania kutafuta soko la Marekani kupitia Oman kwani nchi hiyo ya Falme za kiarabu ina cheti  na kibali kilichothibitishwa na mamlaka ya chakula na dawa cha Marekani, “Tunaweza kuchukua nyama kutoka Tanzania na kuingiza Marekani bila kulipa Ushuru, tunapaswa kuwa na vyeti halali ili kuweza kupata soko katika nchi nyingine, Alisema Waziri Ismail.”
Waziri Ismail aliendelea kusema kuwa, Makampuni Binafsi kutoka Oman yapo tayari kufanya biashara katika eneo hili hivyo ni wakati wa Tanzania sasa kuonyesha utayari.
“Hizi bidhaa za nyama ni lazima zitoke kwenu sababu sisi hatuna maji wala majani ya kulisha mifugo kama ngombe, mbuzi na kondoo ambao huchinjwa kwa wingi baada ya Hijja. Alisisitiza.”
Kwa Upande wa Sekta ya Uvuvi Waziri Huyo wa Oman alisema Oman imenunua teknolojia ya kisasa ya uwekezaji katika fukwe ya Bahari kutoka Texas Marekani, Teknolojia inayojulikana kitaalam kama Shrim farming inayoruhusu uzalishaji wa chakula cha samaki wavuliwao katika maji marefu bila kuharibu mazingira.
Alisema Tenkolijia hiyo inaweza kutumika katika uwekezaji wa Fukwe ya bahari ya Hindi akitolea mfano eneo la bagamoyo kwa kuzingatia tathmini ya athari ya mazingira na ujenzi wa miundombinu ya barabara ili kuwasaidia wavuvi wadogo.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo  Dkt Yohana Budeba Alisema ni furaha yake kuona wafanya biashara wa Oman wanakuja kuwekeza Tanzania au kushirikiana na wavuvi wa ndani kwani kuna samaki wengi wa kutosha kumudu viwanda vya kuchakata  na kuwezesha biashara kubwa ya samaki.
  Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salim Al Ismail, akimtembeza Mhe. Luhaga Mpina Waziri wa Mifugo na Uvuvi katika meli ya Oman baada ya mazungumzo yalohusu sekta ya Mifugo na Uvuvi Dar es Salaam leo.
Majadiliano kati ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salim Al Ismail, na wataalam kutoka pande hizo mbili kuhusu uwekezaji kwenye sekta ya Mifugo na Uvuvi. (Na Mpiga Picha Maalum.)
 Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salim Al Ismail, akimtembeza Mhe. Luhaga Mpina Waziri wa Mifugo na Uvuvi katika meli ya Oman baada ya mazungumzo yalohusu sekta ya Mifugo na Uvuvi Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salim Al Ismail, na wataalam kutoka pande hizo mbili kuhusu uwekezaji kwenye sekta ya Mifugo na Uvuvi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...