Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kinonondoni Mhe. Ally Happy sambamba na uongozi wa Manispaa hiyo kutafuta eneo maalumu litakalofaa kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la kuogelea lenye viwango vya kimataifa litakalotumika kufundishia vijana wa Kitanzania jinsi ya kuogelela. 
Mhe. Jaffo ameyasema hayo wakati wa hafla fupi ya kuangalia eneo la shule litakalofaa kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la kuoegelea litakalofadhiliwa na chama cha kuogelea Tanzania.
Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe alisema kwa kipindi kirefu watanzania tumekuwa tukiungaunga kwenye mashindano mengi ya kimataifa kitu ambacho kimesababisha ushindi wetu kuwa wa kusua sua kila wakati lakini sasa tunataka tuweke miundombinu katika mashule ambayo itatoa fursa ya watoto kujifunza kuogelea kuanzia ngazi za chini.
“Tuna vipaji vingi sana katik Nchi yetu lakini haviendelezwi mfano katika hili la kuogelea kule kwetu Mbeya watu wanaogelea kwenye mito na wanajua vizuri  lakini ukiwaleta kwenye mabwawa ya kimataifa wataishia kushindwa kwa sababu hawana mbinu za kitaalamu za kushiriki kwenye mchezo huo” Alisema Mhe. Makyembe.
Akipokea maombi ya kujenga bwawa la kuogelea katika shule ya msingi Osterbay Waziri wa Tamisemi Mhe. Selemani Jafo amesema amepokea na kukubali ombi la kujenga bwawa la kuogelea lakini eneo la shule ya Osterbay  ni dogo halitakidhi mahitaji na viwango vya bwawa la kimataifa la kuogelea hivyo uongozi wa Manispaa utafute eneo lingine kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.
Aliongeza kuwa anawashkuru wafadhili kutoka Chama cha kuogelea Tanzania kwa kuamua kutoa msaada wa ujenzi wa bwawa la kuogelea ili kukuza vipaji wa watanzania wengi ambao wamekosa fursa hiyo kutokana na ukosefu wa mabwawa ya kuogelea(Swimming Pools) katika maeneo mengi.
Pia amewaomba wafadhili hao kuendeleza kutoa msaada huo Nje ya Mikoa ya Dar es Salaam na kufika mpaka Dodoma katika chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo ambapo pana eneo la kutosha kwa ujenzi wa bwawa la kimataifa na uhitaji ni mkubwa kwa kuwa wanafunzi wanaosoma hapo ni muhimu wakapatiwa burudani (entertainment) mbalimbali baada ya kutoka masomoni.
 Kutoka kushoto ni Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Hapy, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Osterbay wakikagua eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la kuogelea.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo(aliyesimama)akizungumza wakati wa hafla ya kuangalia eneo lililokuwa limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la Kisasa la Kuogelea katika shule ya Msingi Osterbay.
 Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe akizungumza katika hafla ya kuangalia eneo lililokuwa limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la Kisasa la Kuogelea katika shule ya Msingi Osterbay.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo(kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Happy (kushoto) wakati wa wa hafla ya kuangalia eneo lililokuwa limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la Kisasa la Kuogelea katika shule ya Msingi Osterbay.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo(katikati) akiwa na Waziri wa habari, Sanaa na  Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe(tatu kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Happy( nne kulia) na walimu wa shule ya Msingi Osterbay wakati wa hafla ya kuangalia eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la Kisasa la kuogelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...