Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amezungumzia umuhimu kwa wafanyakazi wote waliopata fursa ya kujenga reli ya kisasa (SGR) kufanya kazi kwa moyo na uzalendo mkubwa ili kuandika historia katika maendeleo ya Tanzania.
Profesa Mbarawa amesema hayo alipokagua ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), inayojengwa usiku na mchana kuanzia Dar es Salaam-Morogoro  yenye urefu wa KM 205 na kuzungumzia kuridhishwa na kasi ya ujenzi huo.
“Hii ni fursa kubwa ambayo mmeipata kujenga mradi mkubwa utakaocha historia katika nchi hii hivyo fanyeni kazi kwa bidii, weledi na uzalendo”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Amewataka viongozi wa Shirika Hodhi la Rasilimali za Reli (RAHCO), kuwa katika eneo la mradi wakati wote ili kuhakikisha mkandarasi anapata ushirikiano wa kutosha na hivyo kuwezesha mradi kukamilika kama ilivopangwa.
Aidha amemuagiza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO Mhandisi Edward Malima, kuhakikisha wanafunzi wa uhandisi wanapata nafasi ya kutosha ya kushiriki kwa vitendo katika ujenzi huo ili kuiwezesha nchi kuwa na wataalamu wa kutosha wenye uzoefu kwenye ujenzi na usimamizi wa miradi ya reli.
“Ongezeni wahandisi wanafunzi katika mradi huu, nia yetu ni kupata reli lakini pia na wataalamu wengi katika ujenzi na uendeshaji wa reli”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Naye  Mhandisi Edward Malima, amempongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa kufanya ziara ya kustukiza usiku ambayo imechochea hamasa kwa wafanyakazi na mkandarasi na kuahidi  kumsimamia mkandarasi kikamilifu ili mradi huo ukamilike kwa wakati na uwiane na thamani ya fedha.
Takribani shilingi trilioni 2.8 zinatarajiwa kutumika kujenga reli ya kisasa (SGR), awamu ya kwaza kati ya Dar es Salaam na Morogoro yenye urefu wa KM 205 itakayowezesha treni ya umeme yenye kasi ya KM 160 kwa saa kupita na hivyo kuhuisha mfumo wa usafiri wa reli hapa nchini.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Yapi Merkezi Abdullah Kilic, anayejenge reli ya kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam-Morogoro  yenye urefu wa KM 205 eneo la Soga, mkoani Pwani. 
 Meneja Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Mhandisi Maizo Mgedzi, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, alipokagua ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam-Morogoro yenye urefu wa KM 205 eneo la Soga, mkoani Pwani, inayojengwa usiku na mchana.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akimpongeza mwanamke anayeendesha mtambo wa kutengeneza tuta la reli ya kisasa (SGR), Bi Miriam Juma alipomkuta saa 4 za usiku akichapa kazi katika eneo la Soga, mkoani Pwani.
Muonekano wa Mitambo ya kisasa inayojenga Reli ya Kisasa (SGR), kutoka Dar es Salaam-Morogoro yenye urefu wa KM 205 eneo la Soga mkoani Pwani, inayojengwa kwa saa 24. Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...