Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya nne na Mbunge wa kuteuliwa, Mama Salma Kikwete amezitaka mamlaka zinazojihusisha na utoaji haki, kuwasaidia wanawake kupata haki zao pindi wanapofungua mashauri ya kudai matunzo ya watoto. Amesema hayo Jijini Dar es Salaam wakati wa kongamano la wanawake wanaolea watoto peke yao Single Mothers lililoandaliwa na kituo cha Radio cha Efm na Tv E.
Mama Salma amesema kuwa ni vyema wanaume kutambua majukumu yao ya kulea watoto kwani ni matakwa ya sheria watoto kulelewa na wazazi wote na sio kuwatelekeza  na kusema  watoto wanatakiwa kupata malezi mema  na ya upendo.
"Wanawake wanatekesa wanapotafuta haki zao  kutokana na unyonge na umasikini waliokuwa nao hivyo haki itendeke ili wanawake watembee kwa kujiamini katika nchi yao," amesema Mama Salma.
Aliongeza kuwa watoto wana haki ya kupata malezi mema kutoka kwa wazazi wote, elimu na afya ili kukua vizuri kiakili na kijamii.
"Ukiona wanawake wanatupa watoto jiulize kuna nini, bila tatizo hawawezi kutupa mtoto kwani anauma sana na ndio maana wengine wanapojifungua wanawaviringisha na kuwaweka mahali pazuri  akijua kwamba lazima watu watapita na kumuokota na kwamba atalelewa vizuri," alieleza.
Alisisitiza kuwa wanaume wanapaswa kutambua mazingira ya wake zao pindi wanapokuwa wajawazito na wawatunze, kuwathamini na kuwajali watoto.
Mama Salma alisema wasiwaachie malezi wanawake pekee kwani hakuna mtoto asiye na baba.
Pia alisema kuwa kampeni hiyo ya kuwawezesha wanawake kiuchumi inayofanywa na Kituo cha Redio Efm na TV E inapaswa kuungwa mkono kwani ndio muelekeo wa Siku ya Wanawake duniani inayoadhimishwa kila mwaka Machi 8.
Naye, Mhariri wa kituo hicho cha redio, Scholastica Mazura alisema ni wakati wa kutoa elimu kwa vijana wanaoingia kwenye ndoa ili kupunguza idadi ya watoto wanaolelewa na mzazi mmoja. 
Alisema wanawake wengi wanaishi nje ya ndoa zao  kwa sababu mbalimbali na hivyo tatizo la malezi ya upande mmoja kuwa kubwa nchini.
Alieleza kuwa wanawake wamekata tamaa kwani wapo ambao wametelekezwa nao wanatelekeza watoto lakini wengine wanawalea kwa shida ili wapate malezi bora.
"Tuwacheke wanaume wanaokimbia majukumu yao na kuwaachia wanawake pekee kwa kufanya kazi kwa bidii bila kukata tamaa kwani mnauwezo mkubwa wa kulea nasi tutawasaidia ili mjikwamue kiuchumi," alisema Mazura.
 Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya nne na Mbunge wa kuteuliwa, Mama Salma Kikwete Akicheza na Wanawake waliojumuika katika Tamasha la Single Mothers lililoandaliwa na Efm Radio kwa kushirikia na Tv E
 Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya nne na Mbunge wa kuteuliwa, Mama Salma Kikwete akiwapungia mkono wanawake walioshiriki Tamasha la Sinle mothers wakati anaingia ukumbini
 Mbunge wa Viti Maalum Catherine Magige akizungumza na kuwatia moyo wanawake hao na kusema pia hata yeye ni Single Mothers na bado maisha yanenda
 Mhariri wa kituo hicho cha redio Efm na Tv E, Scholastica Mazura akizungumza  na vijana wanaoingia kwenye ndoa ili kupunguza idadi ya watoto wanaolelewa na mzazi mmoja. 
 Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya nne na Mbunge wa kuteuliwa, Mama Salma Kikwete akipoke Zawadi kutoka kwa Meneja Tukio wa Efm na Tv E , Jesca Mwanyika.
 Mbunge wa Viti Maalum Rita Kabati akizungumza na wnawake wanaolea Watoto peke yao juu ya umuhimu wa kumtegeea Mungu hili kufanikiwa
 Waziri Mstaafu na Mbunge , Hawa Ghasia akieleza ugumu wa kulea mtoto peke yako na kuwatia moyo wanawake wote waliotelekezwa
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya nne na Mbunge wa kuteuliwa, Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Efm Radio na Tv E ambao ni Single Mothers 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...