Na Fredy Mgunda,Mufindi Kaskazini.

Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini ametoa jumla ya bati mia tano tisini (590) na saruji mifuko mia mbili ishirini (220) kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa madarasa ya shule,zahanati na nyumba za wafanyakazi wa zahanati na walimu wa shule zilizopo katika kata ya Ihalimba huku lengo likiwa kuboresha sekta ya elimu na afya kwa wananchi. 

Akizungumza na walimu wa kata hiyo mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmuod Mgimwa alisema kuwa ameamua kuwekeza katika elimu na afya kwasababu wananchi wakifanikiwa kupata vitu hivyo viwili kwa wakati watafanya maendeleo kwa kasi kubwa kulingana na wakati uliopo na kuendana na mazingira wanayoishi.

“Hivi ndio vipaumbele vyangu kwa kijiji hiki kwa wakati huu maana nimegundua kuwa changamoto kubwa ni kuwa shule nyingi za msingi zilijengwa miaka mingi iliyopita sasa zimechakaa na sio rafiki kwa wanafunzi kuwasaidia kupata elimu bora hivyo nimeanza na hilo pamoja na kuchangia maendeleo kwa kuboresha sekta ya afya ili wananchi wakiugua waweze kutibia hapa hapa kijiji kwa kuwa nina uhakika huduma itakuwa inatolewa kwa ustadi mkubwa na yenye ubora unaotakiwa” alisema Mgimwa
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na walimu juu ya mambo aliyoyafanya kwenye kata hiyo kielimu ambapo ametoa jumla ya bati mia tano tisini (590) na saruji mifuko mia mbili ishirini (220) kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa madarasa ya shule,zahanati na nyumba za wafanyakazi wa zahanati na walimu wa shule zilizopo katika kata ya Ihalimba
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiwa na viongozi wa elimu ngazi ya wilaya kata na vijiji wakati wa mkutano baina ya viongozi hao na walimu wa shule za kata ya Ihalimba
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akimkabidhi zawadi mmoja ya mwalimu aliyefanya vizuri darasani kwa kuongeza ufaulu 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...