Na Anitha Jonas – WHUSM
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Duniani (FIFA) Bw.Gianni Infantino atafanya mkutano wa majadiliano na vyombo vya habari kumi na mbili vya ndani ya nchi.
Taarifa hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe katika mkutano na wahariri wa habari za michezo uliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
‘’Huu ni utaratibu wa viongozi wa FIFA kufanya mkutano wa mazungumzo na waandishi wa vyombo vya habari katika nchi wanazofanyia mikutano yao  ya kikazi kama ulivyo mkutano huu wanaotarajia kuufanya nchini Februari 22,mwaka huu,’’alisema Dkt. Mwakyembe.
Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo Waziri Mwakyembe alieleza kuwa Rais wa FIFA Bw. Gianni Infantino anatarajia kuwasili nchini alfajiri ya saa nane usiku kuamkia Februari, 22 2018 ambayo ndiyo siku ya mkutano na saa tatu asubuhi yake ataelekea ikulu kukutana na viongozi wakuu wa nchi.
Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Bw.Wilfred Kidau alitoa ufafanuzi kuhusu mkutano huu wa viongozi wa FIFA na CAF kuwa umebeba ajenda mbalimbali  ikiwemo kujadili kuhusu Maendeleo ya Soka la Wanawake,Maendeleo ya Soka la Vijana,Utaratibu wa kusaidia Vilabu vya soka pamoja na vipaumbele mbalimbali vya kukuza soka kwa nchi za Afrika.
‘’Mkutano huu wa FIFA unatarajia kufanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam (JNICC) na ni sawa na kikao cha ndani ambacho kimelenga zaidi kujadili masuala ya maendeleo ya shirikisho hilo kwa ajili ya kuandaa agenda za mkutano mkuu wa FIFA wa dunia hivyo ombi kwa waandishi wa habari ni kuelewa dhana ya mkutano siyo kuwa wamenyimwa fursa bali huo ndiyo utaratibu’,’alisema Bw. Kidau.
Pamoja na hayo Bw.Kidau alifafanua kuwa miongoni mwa vyombo vitakavyopata fursa ya kushiriki majadiliano hayo baadhi yao watarusha mazungumzo hayo mubashara katika vyombo vyao hivyo wadau wengine wataweza kufuatilia tukio hilo moja kwa moja kupitia vyombo hivyo.
Halikadhalika Rais huyo wa FIFA anatarajia kuondoka nchini jioni mara baada ya kumaliza mkutano mwake na kushiriki chakula cha jioni.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (wa kwanza kushoto) akitoa ufafanuzi wa idadi ya waandishi watakaohitajika katika mkutano wakati wa mkutano wa  majadiliano na Rais wa Shirikisho la Mipira wa Miguu Duniani (FIFA) Bw.Gianni Infantino utakaofanyika mnamo Februari 22, Mwaka huu na waandishi wa habari, katika mkutano wake na Wahariri wa Habari za Michezo (hawapo pichani) nchini leo jijini Dar es Salaam,Katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi Suzan Mlawi na Kulia ni Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw.Wilfred Kidau
 Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Bw.Wilfred Kidau akitoa ufafanuzi kuhusu ajenda za mkutano wa Rais wa Shirikisho la Mipira wa Miguu Duniani (FIFA) na CAF utakaofanyika nchini Februari 22,2018 katika mkutano na  Wahariri wa Habari za Michezo nchini  (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa Habari kutoka Gazeti la Nipashe Bi Somoe Ng’itu akiuliza swali kuhusu utaratibu wa waandishi wa habari watakaofika Ikulu kuripoti tukio la Rais wa Shirikisho la Mipira wa Miguu Duniani (FIFA) kukutana na viongozi wakuu wanchi, kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani ) leo jijini Dar es Salaam katika mkutano wa wahariri wa habari za michezo nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...