SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imesema itamchukulia hatua kali mtu yoyote atakayebainika kuhujumu utekelezaji wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Mkoani humo wenye gharama ya bilioni 600 kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa eneo hilo.

Kauli hiyo imetolewa leo wilayani Nzega na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wakati alipotembelea na kukagua mradi huo unaotoa maji katika Kijiji cha Solwa mkoani Shinyanga kupeleka mkoani Tabora ambapo wilaya za Nzega, Igunga, Uyui na Tabora mjini zitanufaika na mradi huo wa maji kutoka ziwa Victoria unaotekelezwa kwa muda wa miezi thelathini.

Alisema kuwa Serikali haitamfumbia macho mtu yeyote atakayebainika kuwa na nia ovu ya kutaka kuiba vifaa mbalimbali ambavyo vinatumiwa na wakandarasi katika kujenga mradi huo ambao ni muhimu sana kwa ajili ya wakazi wa maeneo mbali ya Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akizungumza na Mkandarasi na wananchi baada ya kutembelea na kukagua mradi wa maji kutoka ziwa Victoria jana ambapo mradi huo unaotoa maji katika Kijiji cha Solwa mkoani Shinyanga kupeleka mkoani Tabora ambapo wilaya za Nzega,Igunga,Uyui na Tabora mjini zitanufaika na mradi huo wa maji kutoka ziwa Victoria unaotekelezwa kwa muda wa miezi thelathini. 

Mwanri alisema kuwa hadi sasa kazi inaendelea ambapo Mkandarasi ya kampuni ya L & T yupo kazini akiendelea na shughuli ya kuunga na kufukia mabomba ardhini na kueleza kuwa hujuma yoyote ambayo inaweza kujitokeza inaaweza kusababisha mradi kuchelewa kumalizika kusababisha wakazi wa maeneo ambao yalikuwa yapate huduma hiyo kuendelea kupata matatizo ya maji.

Alisema kuwa kama kuna matatizo yoyote wanayopata kama vile wizi wa vifaa ni vema wakaeleza ili uongozi wa Mkoa uweze kuchukua hatua mapema kwa ajili ya kuendelea kuwawekea mazingira mazuri ya ujenzi wa mradi huo na kuongeza kuwa kama watapata matatizo na kunyamaza na muda wa kukamilisha mradi utafika wakiwa bado hawajakamilisha Serikali haitasikiliza.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari baada ya kuungana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora (hayupo pichani) kutembelea na kukagua mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria jana ambapo mradi huo unaotoa maji katika Kijiji cha Solwa mkoani Shinyanga kupeleka mkoani Tabora ambapo wilaya za Nzega,Igunga,Uyui na Tabora mjini zitanufaika na mradi huo wa maji kutoka ziwa Victoria unaotekelezwa kwa muda wa miezi thelathini.

Mwanri aliwataka Wakuu wote wa Wilaya na Watendaji wote ambapo mradi huo unapita kuhakikisha wanasimamia ili isije ikatokee hujuma yoyote na kama ilitokea wakamate watu wote wanatuhumiwa.

Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Mkama Bwire alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo upo ndani ya utekelezaji na tayari hata malipo ya fidia kwa wananchi  waliopitiwa maeneo yao na mradi yamekwishafanyika. Alisema wananchi 204 ambao maeneo yanapitiwa na Mradi huo na kukabainika kuwa wanatarajiwa kulipwa milioni 890.5 zitatumika  kama fidia  kwa wananchi hao

Alisema kuwa jumla ya milioni 760 zimeshalipwa kwa wananchi zaidi ya 162 ambao maeneo yao yalikwishafanyiwa tathmini.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Nzega alisema wananchi wa wilaya yake wanaupokea Mradi huo kwa furaha kwa kukamilika kwake kutasaidia kuwaondolea tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama ya uhakika. Mradi huu wa Maji unatarajia kuwanufaisha wakazi wa Mkoa wa Tabora wapatao milioni moja ambao watakuwa na uhakika wa maji safi na salama.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na Taka Manispaa ya Tabora (TUWASA) Mkama Bwire akitoa ufafanuzi juu ya ulipaji fidia wakati utekelezaji wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria jana mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri kutembelea na kukagua mradi huo.
Baadhi ya Mafundi wa Kampuni ya L & T wakiwa kazini wakiendelea na shughuli ya kuunga na kufukia mabomba ardhini kwa ajili ya kupeleka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Tabora.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...