Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Antwerp Ubelgiji na Chuo Kikuu cha Kikristu cha Uganda ambao wapo katika programu ya kubadilishana Wanafunzi na Chuo kikuu Mzumbe wamewasilisha matokeo ya awali ya tafiti walizofanya kwenye maeneo ya maji, elimu na usalama wa chakula kwa kusimamiwa na wahadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe ikiwa ni sehemu ya mafunzo yao katika Shahada ya Umahiri ya Menejimenti ya ufuatiliaji na Tathmini.

Akizungumza katika semina ya uwasilishaji wa matokeo ya tafiti hizo iliyofanyika Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi

Kuu Morogoro mwishoni mwa wiki, Mratibu wa Mradi wa ‘ICP connect’ unaotekelezwa kwa ushirikiano baina ya Chuo kikuu Mzumbe na Chuo Kikuu cha Antwerp, Ubelgiji Dkt. Christina Shitima amesema kuwa uwasilishaji wa matokeo ya tafiti hizo ni matunda ya mkataba wa ushirikiano kati ya Chuo Kikuu Mzumbe na Chuo Kikuu cha Antwerp vilivyokubaliana kushirikiana na kubadilishana wanafunzi na wanataaluma, kutengeneza programu pamoja na kufanya tafiti

Dkt. Shitima amesema kuwa uwasilishaji wa matokeo hayo ya awali umelenga kuisaidia Serikali na Wadau kuchukua hatua madhubuti ikiwemo kutunga sera na kufanya maamuzi ya kuboresha huduma za kijamii zikiwemo maji, elimu na usalama wa chakula ambazo tafiti zake ndio zinatolewa mrejesho na wanafunzi hao.

Katika hatua nyingine, wadau mbalimbali walioshiriki katika Semina hiyo ya kutoa matokeo ya awali wameeleza kuwa tafiti hizo zitaisaidia Serikali kuandaa vyema malengo, mipango na bajeti kwa ajili ya kuzitatua changamoto zilizoibuliwa na watafiti hao na hatimaye kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi

“Tafiti hizi zina tija kubwa sana ikiwa zitawasilishwa kwa Serikali na mamlaka zenye dhamana kwani zitasaidia kuweka mipango bora ya kuzikabili changamoto zilizoibuliwa katika sekta ya maji, elimu na chakula. Hata hivyo, tayari Serikali imeshaanza kuchukua hatua katika bajeti inayokuja kwa kuweka mipango ya kuboresha miundombinu ya shule ya msingi ya Mongwe ambako ilikuwa ni moja ya sampuli za utafiti kwenye sekta ya elimu”. Alisema Diwani wa Kata ya Mlali Mhe. Frank Mwananzeche.

Naye Mhandisi wa Mamlaka ya Maji Wilaya ya Mvomero Mhandisi Mlenge Luperitilo amesema tafiti kama hizo zinawasaidia wao kama watendaji wa Serikali kubaini changamoto kwenye maeneo ambayo yana shida zaidi na pengine wameshindwa kuyafikia kwa wakati huo na hivyo kuwekeza nguvu zaidi katika kutatua changamoto za maji.

Mhandisi Mlenge amekishukuru Chuo Kikuu Mzumbe kwa kuwazesha wanafunzi hao kufanya tafiti hizo na amewaomba watafiti wengi zaidi kujitokeza ili kushirikiana na Serikali kutatua changamoto mbalimbali za wananchi hasa kwenye sekta ya maji.

Kwa upande wao Wanafunzi hao wa kimataifa wamesema wamefurahi kupata fursa ya mafunzo ya kufanya tafiti nchini Tanzania kupitia Chuo Kikuu Mzumbe ambacho wamekielezea kuwa ni chuo bora sana kwa masomo kwani kina mazingira mazuri na tulivu ya kujifunzia na kwamba wanaamini matokeo ya tafiti waliyoyawasilisha yataisaidia Serikali na Wadau kuboresha huduma, na hivyo watakuwa wametoa mchango wao wa kimaendeleo.

“Tumekaa hapa Chuo Kikuu Mzumbe kwa wiki tano za mafunzo, tumekuwa na wakati mzuri sana katika mafunzo ya darasani, tumepata fursa ya kubadilishana uzoefu na wanafunzi wenzetu, tumetembelea vijiji na kuzungumza na wanajamii tumepewa ukarimu wa hali ya juu na wenyeji wetu kuanzia waratibu, walimu na wanafunzi.Tumefurahi sana kujifunza Chuo Kikuu Mzumbe”. Alisema Fiona Ward Shaw, raia wa Marekani na Mwanafunzi wa Shahada ya Umahiri katika Menejimenti ya Tathmini na Ufuatiliaji anayesoma Chuo Kikuucha Antwerp kilichopo nchini Ubelgiji.

Naye Vicent Manimani raia wa Congo DRC na Mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Kikristu cha Uganda amesema wamepata uzoefu wa kutosha utakaowasaidia katika taaluma yao na amewakaribisha wanafunzi wengine kutafuta fursa ya kutembelea na kujifunza katika Chuo kikuu Mzumbe kwa kuwa ni chuo kizuri sana.

“Mzumbe ni njema sana kwa kujifunzia, ninawakaribisha watu wengine kutembelea na kujifunza hapa, hakuna matata”. Alisema Vicent Manimani.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Daniel Chongolo ameipongeza timu ya wataalamu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kwa kufanya kazi kwa haraka na ufanisi mkubwa kuhakikisha barabara zinapitika mkoani Songwe.

RC Chongolo ameeleza kuwa changamoto ya uharibifu mkubwa wa miundombinu umefanyiwa kazi kwa haraka na timu ya wataalamu wa TANROADS na TARURA jambo ambalo limerejesha mawasiliano ya pande zote zilizokuwa hazipitiki.

"Kila mmoja kwa barabara zake wamefanya kazi kubwa na wanaendelea kufanya hivyo lengo ni kuhakikisha Wananchi hawakosi huduma ya barabara pale inapotokea changamoto’’ Amekaririwa Mhe Chongolo.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Songwe Mhandisi Suleiman Bishanga akizungumza mara baada ya kukagua sehemu zilizoathirika na mvua za El-Nino wilayani Songwe na Ileje amesema kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 5.7 kwa ajili ya kutatua changamoto na kurejesha miundombinu ya barabara na madaraja ambayo yameharibiwa na mvua kubwa za El- nino zinazoendelea kunyesha Mkoani Songwe.

Amesema kuwa Wilayani Songwe miundombinu imeharibika katika barabara ya Galula – Namkukwe sehemu ya Malangali, daraja la Mpona maji yalifurika juu na kukata mawasiliano kati Kijiji cha Namkukwe na Mpona.

Sehemu nyingine ni Magamba eneo linalounganisha Kijiji cha Mpona na Igalula ambako sasa hivi linajengwa daraja na kuinua tuta la barabara; pia kwenye barabara ya Chang’ombe - Mkwajuni eneo la Zira miaka ya nyuma lilikuwa korofi; lakini mwaka huu halijapata changamoto kwa sababu Serikali kupitia TANROADS ilichukua hatua za mapema kulifanyia matengenezo.

Ameeleza kuwa Wilayani Mbozi Barabara iliyoathirika zaidi ni Mlowo – Kamsamba ambayo inaunganisha Mji wa Songwe kuelekea upande wa Mkoa wa Rukwa ambapo Serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni moja kutengeneza maeneo mbalimbali yaliyoharibika.

“Katika Wilaya ya Momba kuna barabara ambayo tumeirithi mwaka jana kutoka TARURA kuja TANROADS na yenyewe ilikuwa katika hali mbaya, Serikali haikusita ikatupa fedha shilingi milioni 500 ambazo zimeenda kushughulikia matatizo ya kule na sasa ile Barabara ya Kwenda Ilonga inapitika’’ ameeleza Mhandisi Bishanga na kuogeza.

“Wilaya ya Mbozi kuelekea Ileje kuna sehemu tunaunganishwa na Daraja la Hezya lile dadaja lilisombwa na maji na Serikali imetoa zaidi ya shilingi milioni 261 kwa ajili ya kujenga daraja hilo na kwa sasa linapitika’’.

Kwa upande wao Afisa Tarafa ya Songwe Godwin Kaunda na Diwani kata ya Magamba Mhe Kapala Chakupewa Makelele wameishukuru serikali kupitia TANROADS kwa urejeshaji wa haraka kwa miundombinu ya barabara na madaraja iliyoathiriwa na mvua za El-Nino zinaendelea kunyesha katika maeneo mengi nchini.









Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akizungumza katika sherehe za jumuiya ya Wazazi zilizofanyika kiwilaya katika Kijiji cha Kilagano Halmashauri ya wilaya Songea.Na Maandishi wetu
WAZIRI  wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho amewataka wazazi kutenga muda malezi kwa watoto ili kuwatizama na Kurekebisha mienendo yao.

Kauli hiyo ameitoa mapema Leo tarehe 05/05/2024 Wakati aliposhiriki kama Mgeni rasmi maadhimisho ya miaka 69 ya Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Songea Vijijini, sherehe zilizofanyika katika Kijiji cha Kilagano katika Halmashauri ya wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.

Waziri amesema, mtoto anayelelewa kwa kuangalia mfano mzuri wa baba na mama lazima atakuwa na nidhamu na tabia njema.

"Wazazi tukae tutafakari utaratibu tunaotumia kulea watoto wetu ili wawe na madili bora katika katika Jamii,"alibanisha.

Ameeleza kwamba lengo la kuanzishwa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi ni kuhakikisha inajenga maadili mema ndani ya chama na taifa kwa ujumla.

Niendelee kuhimiza Viongozi wa jumuiya ya wazazi ndani ya wilaya kwenye Kata na kwenye matawi na kwenye Mashina tuendelee kulibeba jukumu hili.

"Kizazi kilichopo na hata kizazi kipya kimeathirika na maswala ya utandawazi, na nguvu mpya ya Mawasiliano kama isipotumika vizuri itakuwa ni chanzo cha upotofu wa maadili," alisema Waziri Mhagama.

Tunahitaji wanachama wenye maadili, tunahitaji wananchi wa Peramiho wenye maadili, alifafanua.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini Mhe. Menace Komba ameishukuru Serikali na juhudi za Mhe. Mbunge Mhe. Jenista Mhagama, walizofanya za kurekebisha Mpaka wa Mlima Lihanje.

Tulifanya Mkutano na timu ya Mawaziri na tulifanya Mkutano Kilagano na kuzungumza na wananchi na baadae kufanikiwa kurekebisha mipaka ya Mlima Lihanje.

"Serikali ya wilaya itahakikisha wananchi walioathirika na zoezi hilo kwa kuondolewa kwenye Mlima na kuwarudisha chini wanapata ardhi iliyotengwa kwa usawa," alisema.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akifurahia Jambo na Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi katika sherehe yao iliyofanyika kiwilaya katika Kijiji cha Kilagano Halmashauri ya wilaya ya Songea.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu ) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa jumuiya ya Wazazi mara baada ya kuhitimisha sherehe yao iliyofanyika katika Kijiji cha Kilagano Halmashauri ya wilaya ya Songea.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akifurahia Jambo na wakinamama walioshiriki kutumbuiza sherehe za Jumuiya ya Wazazi za Chama Cha Mapinduzi zilizofanyika kiwilaya Katika Kijiji cha Kiagano Halmashauri ya wilaya ya Songea.
Mratibu wa mafunzo (Supervisor Learning and Development wa Barrick Tanzania,Elly shimbi akiongea na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakati wa kongamano lakuwajengea uwezo wakujiamini na kuhimili ushindani wa ajira na kujiajiri lililoandaliwa na taasisi ya AIESEC Tanzania lililofanyika katika chuo hicho mwishoni mwa wiki kwaudhamini wa Barrick.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma na vyuo vya elimu ya juu mkoani humo wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa kongamano hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa ,Mayeka Simon Mayeka akiongea katika kongamano hilo.

Na Mwandishi Wetu.

Kampuni ya madini ya Barrick nchini, imedhamini na kushiriki katika kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma na Iringa lililoandaliwa na taasisi ya kuchipua na kuendeleza vipaji vya uongozi kwa vijana (AIESEC Tanzania) lililofanyika katika vyuo hivyo na kuwashirikisha wanafunzi wanaosoma vyuo vya elimu ya juu,wahadhiri na wadau mbalimbali.

Kupitia makongamano haya ambayo hufanyika kila mwaka, wanafunzi huweza kufahamu jinsi taasisi mbalimbali nchini zinavyoendesha shughuli zake lengo kubwa ikiwa ni kuwajengea uwezo wa kujua vipaji walivyonavyo, kujifunza jinsi ya kujiamini na kukabiliana na ushindani katika soko la ajira,kujiamini kwa kujiajiri,kuchangamkia fursa zinazojitokeza na kujitambua uwezo wao ni jinsi gani wanaweza kushiriki kutoa mchango wa kuendeleza taifa pindi wamalizapo masomo yao.

Maofisa Raslimali Watu Waandamizi na wataalamu mbalimbali kutoka Barrick pia walishiriki katika maonesho na kongamano hayo ambapo walipata fursa kuzungumza na wanafunzi kuhusiana na kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ajira,kuendeleza vipaji vyao pia wanafunzi walipata fursa kuelewa jinsi kampuni ya kimataifa ya dhahabu ya Barrick, inavyoendesha shuguli zake kwa kutoa kipaumbele kusaidia jamii sambamba na mpango wake wa kuibua na ukuzaji wa vipaji kwa vijana wa kitanzania,kuwezesha wanawake kuingia katika sekta na wafanyakazi wake.

Wanafunzi kutoka vyuo hivyo walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali kuhusiana na ajira kwa wataalamu wa fani ya Raslimali kutoka makampuni mbalimbali walioshiriki katika makongamano hayo.

Akiongea katika kongamano lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa ,Mayeka Simon Mayeka ambaye alikuwa mgeni rasmi aliwataka wanafunzi kujiamini wakati wote na kuchangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza zikiwemo za ajira na kujiajiri.
Alisema zama hizi na maisha ya kidigitali vijana wanayo nafasi kubwa kupata mafanikio iwapo wataandaliwa vizuri.Alipongeza taasisi ya AIESEC Tanzania kuandaa makongamano ya kuwajengea uwezo wanafunzi vyuoni pia aliipongezakampuni ya Barrick kwa kudhamini makongamano haya.
Wataalamu kutoka Barrick wakiongea katika kongamano la wanafunzi wa Chuo kikuu cha Iringa lililoandaliwa na na taasisi ya AIESEC Tanzania lililofanyika katika chuo hicho mwishoni mwa wiki kwa udhamini wa Barrick.


Mkuu wa Tawi la Utawala JKT na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akiondoa kitambaa tayari kuzindua Mahanga 15 ya Vijana katika Kikosi 825 KJ Mtabila, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma.
Mkuu wa Tawi la Utawala JKT na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mahanga 15 ya Vijana katika Kikosi 825 KJ Mtabila, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma.
Mkuu wa Tawi la Utawala JKT na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akikagua vitanda mara baada ya kuzindua Mahanga 15 ya Vijana katika Kikosi 825 KJ Mtabila, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma.
Mkuu wa Tawi la Utawala JKT na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua Mahanga 15 ya Vijana katika Kikosi 825 KJ Mtabila, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma. Kamanda Kikosi 825 KJ, Mtabila Luteni Kanali Patrick Ndwenya,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzinduliwa Mahanga 15 ya Vijana katika Kikosi 825 KJ Mtabila, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma.
Na.Alex Sonna_KASULU
MKUU wa Tawi la Utawala JKT na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Brigedia Jenerali Hassan Mabena, amezindua Mahanga 15 ya Vijana katika kikosi cha Jeshi 825 KJ Mtabila kilichopo Kasulu mkoani Kigoma huku akiishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu katika vikosi vya JKT.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mahanga hayo Bregidia Jenerali Mabena alisema kila mwaka serikali imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya shughuli mbalimbali zikiwemo za ujenzi na ukarabati wa miundombinu katika vikosi.
Bregidia Jenerali Mabena,alisema kuwa mahanga hayo yana uwezo wa kuchukua wanafunzi 100 kwa kila hanga moja na kufanya ongezeko la vijana 1500 kwenye kikosi hicho.
"Mahanga haya yanaleta maana kubwa kwa sababu lengo la mafunzo haya kwanza ni kuwafikia vijana wote wa kundi la lazima waliomaliza kidato cha sita na vijana wengine kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria ili kuweza kuwapata vijana wote kuhudhuria mafunzo ya uzalendo ,kulipenda Taifa lao,kuwaweka pamoja na kuondoa tofauti dhidi yao .
Aidha ameishukuru serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na Amiri Jeshi Mkuu kwa kuona umuhimu wa mafunzo hayo ambapo katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake wa wameendelea kupata fedha ambazo wamekuwa wakizielekeza kwenye vikosi vya JKT kuhakikisha wanakwenda kuongeza idadi na hatimaye kuchukua vijana wengi kwa wakati mmoja na kuwaweka pamona.
"Nchi yetu ni kubwa ina watanzania zaidi ya milioni 60 kwa hiyo vijana wa kitanzania wamezaliwa maeneo mbalimbali hivyo unapowaweka pamoja kuwaelekeza utamaduni wa nchi yao inakuwa ni jambo jema sana"alisema na kuongeza kuwa
"Niendelee kuipongeza Serikali lakini zaidi niwapongeze makamanda vikosi kwani wameweza kuielewa vyema ile nia thabiti ya Makao Makuu ya JKT,wizara ya Ulinzi na JKT na Taifa kwa ujumla la kuwaweka vijana hao pamoja na kutekeleza maagizo hayo kwa vitendo."
Akizungumza kwa niaba ya wahitimu JKT katika kikosi cha 825 KJ Amina Singano alisema kama vijana,watayatunza majengo hayo ili yaweze kufumu kwa muda mrefu.
AIRTEL MONEY TANZANIA imetangaza kutoa kiasi cha bilioni 3,956,681,813 TZS kama Gawio la Faida la Airtel Money zitakazogawanywa kwa Wateja na Mawakala wa Airtel Money nchi nzima ambao wamekuwa wakitumia huduma za Airtel Money kati ya Julai hadi Desemba 2023.

Utoaji wa Gawio la Faida ya Airtel Money ni uthibitisho wa kuendela kufanikiwa kwa mikakati ya Airtel money katika kuboresha huduma za kifedha kupitia Airtel Money ili kutoa huduma bora, zenye ubunifu na nafuu kwa wateja. Gawio la Faida la Airtel Money linagawanywa kwa wateja na Mawakala kuanzia sasa.

Gawio la Faida ya Airtel Money hutolewa kwa wateja na mawakala wa Airtel Money kila robo ya mwaka kulingana kiasi na alichoweka kwenye akaunti yake ya Airtel Money. Kiasi cha gawio anachopata kitawekwa moja kwa moja kwenye akaunti ya Airtel Money.

Wateja wa Airtel Money wataweza kutumia kiasi cha gawio la faida ya Airtel Money wapendavyo ikiwemo kujinunulia muda wa maongezi, kutoa kwa wakala au kulipia bili kama vile DAWASCO, LUKU, na nyinginezo.

Airtel Money ilianza kugawa gawio la faida tangu mwaka 2015 ambapo hadi leo imeshagawa jumla ya bilioni 52 kwa wateja na mawakala wake nchini nzima.

"Airtel Money Tanzania tutaendea kutekeleza dhamira yetu ya kutoa huduma nafuu na kuleta mifumo bora ya kupanua miundombinu ya huduma zetu ili kuendelea kusambaa na kutoa huduma vijijini na mjini,” alisema Andrew Rugamba, Mkurugenzi wa Airtel Money.

Aliongeza "Airtel Money tutaendelea kupanua zaidi mtandao wa mawakala ili kuhakikisha huduma zote za Airtel Money zinapatikana kwa urahisi kwa wananchi walio wengi."

Airtel inajivunia miundombinu yake ya usambazaji ya Airtel Money nchini, ambapo ina zaidi ya Airtel Money Branch 4,000 pamoja na mawakala wa Airtel Money zaidi ya 250,000 nchi nzima. Vilevile, Airtel Tanzania imejiunganisha na mifumo ya malipo kielektroniki, ikiwemo ya serikali ili kuwawezesha wateja kufanya malipo mbalimbali ya serikali wakiwa popote.

Airtel Money pia imeunganishwa na zaidi ya benki 40 nchini, hivyo kuwawezesha wateja wa Airtel Money kufanya miamala ya kifedha kutoka kwenye akaunti zao za benki kwenda kwenye akaunti zao za Airtel Money kwa urahisi, huku wakifurahia kutuma pesa kwa wateja wa Airtel bila gharama yoyote.

Airtel Money Tanzania inaendelea kujizatiti katika kuboresha huduma za kifedha kupitia simu kwa wateja wake na itandelea kubuni huduma mbambalia kutokana na mahitaji ya wateja wake na watanzania kwa ujumla ili kuendelea kutoa suluhisho la huduma za kifedha kidijitali na kuondoa changamoto ya kutofikiwa na huduma za kifedha popote nchini.

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), imeingia makubaliano ya kupeleka marubani wake kufundisha na kusimamia ndege mpya za Airbus A220 za Kampuni ya Ndege ya Ibom iliyopo nchini Nigeria.

Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Mha. Ladislaus Matindi, amethibitisha kuwepo kwa makubaliano hayo ambapo amesema ATCL imetoa marubani wake waandamizi wawili ambao watakuwa na jukumu la kuwafundisha kwa vitendo marubani na walimu wa marubani wa Ibom Air kwa muda wa miezi sita.

"Marubani wa ATCL watakuwa na jukumu la kufundisha na kusimamia mafunzo kwa vitendo hadi watakapojiridhisha kuwa marubani wanafunzi na walimu wao wamefikia viwango vinavyotakiwa kurusha ndege hizo", alisema Mha. Matindi.

Aidha, Kampuni ya Ibom Air itailipa ATCL gharama za mafunzo hayo kwa mujibu wa mkataba kwa kipindi chote cha makubaliano.

Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya ATCL kuonesha uzoefu wa muda mrefu wa kumiliki ndege za Airbus A220-300 na pia kuridhishwa na kiwango cha umahiri wa marubani wa Air Tanzania.

Mafunzo hayo yanalenga kujenga uwezo kwa marubani wa Ibom Air watakaorusha ndege za Airbus A220, ambazo ATCL ina uzoefu wa miaka mingi wa kumiliki ukilinganisha na Ibom Air ambao ndio wanaanza kutumia ndege za aina hiyo.

ATCL ina zaidi ya marubani 100 na inamiliki ndege aina ya Boeing B787-8, B737 MAX 9, B767-300F, Airbus A220-300 pamoja na Dehaviland Q400 na Q300.
Marubani waandamizi wa Kampuni ya Ndege Tanzania Kept. Sajjad Moloo na
Kept. Arif Jinnah (kulia na kushoto) wakiwa ndani ya ndege kwa ajili ya mafunzo kwa walimu na marubani wa ndege ya Ibom, nchini Nigeria




Marubani waandamizi wa Kampuni ya Ndege Tanzania Kept. Sajjad Moloo na
Kept. Arif Jinnah (kulia na kushoto) wakiwa ndani ya ndege kwa ajili ya mafunzo kwa walimu na marubani wa ndege ya Ibom, nchini Nigeria

UKISIKIA Bosi kacheka ujue Maokoto yanafuatia, Kupitia promosheni pendwa ya Expanse iliyopo Meridianbet Kasino ya Mtandaoni unaweza kujishindia zawadi kibao, cha kufanya Jisajili Meridianbet kisha cheza shindano la Expanse ushinde.

Mtoa huduma wa michezo ya kasino ya mtandaoni Expanse Studio anashirikiana na Meridianbet kuwaletea shindano kubwa la zawadi, mgao wa Mamilioni unakusubiri, kwa kucheza michezo ya sloti na kasino ya Mtandaoni unajiweka kwenye nafasi ya kushinda, cheza kwa dau la kuanzia ni Tsh 400/=

Kanuni za Shindano la Expanse Kasino ya Mtandaoni
Promosheni hii imeanza 04.05. 2024 hadi Mei 17 ambapo bonasi za kasino zitagawiwa kwa washindi watakaokuwa wanatangazwa kila siku, baada ya kucheza moja kati ya michezo ya kasino ya mtandaoni iliyopo Meridianbet kutoka Expanse studio.

Promosheni ni halali kwa wachezaji waliosajiliwa kwenye APP na tovuti ya meridianbet.co.tz
Promosheni itafanyika katika mtindo wa mashindano kwa wachezaji kwenye sloti zinazotolewa na Expanse Studio. Michezo ya kasino ya mtandaoni itakayotumika wakati wa promosheni ni:

Battle of Egypt
Forest Rock
Fortune Farm
Lucky's Betting Shop
Maya's Treasure
Piggy Party
Spinning Buddha
Sticky 777
The Book of Eskimo
Veni Vidi Vici
Wild Corrida
Zombie Apocalypse
Battle for the Throne
Bounty Hunters
Capital City Derby
Casino Heist
Fairy in Wonderland
Odd One Out
Planet Power
Shaolin Crew

Wachezaji watashindana kwa mfumo wa pointi ambapo kila dau la jumla ya TZS 2,500 litatoa pointi 2. Dau la chini kwa kila mzunguko kwa promosheni hii ni TZS 400.

Kulingana na msimamo wa mwisho, wachezaji 40 watazawadiwa pesa taslimu na mizunguko ya bure kucheza kwenye kasino ya mtandaoni kama ifuatavyo:

Nafasi ya 1 – TSH 2,500,000
Nafasi ya 2 - TSH 1,500,000
Nafasi ya 3 – TSH 500,000
Nafasi ya 4 na 5 - TSH 250,000 kila mmoja
Nafasi ya 6 mpaka 10 – Mizunguko 300 ya bure kwenye sloti ya PIA
Nafasi ya 11 mpaka 20 - Mizunguko 200 ya bure kwenye sloti ya PIA
Nafasi ya 21. mpaka 30 - Mizunguko 100 ya bure kwenye sloti ya PIA
Nafasi ya 31. mpaka 40 - Mizunguko 50 ya bure kwenye sloti ya PIA

Ushindi utakaotokana na Mizunguko ya bure utahitaji kuzungushwa mara 60x (kwa mfano, ukishinda TZS 10,000 kwenye Mizunguko ya bure, utahitaji kucheza TZS 600,000 kwenye mchezo uleule ili kuhamisha ushindi wako kwenye akaunti ya pesa halisi).

Taarifa kuhusu malipo ya juu kwa kila Kundi la Mizunguko ya bure, washindi watapokea taarifa ambayo itatumwa kwao si zaidi ya saa 13:00 AM tarehe 18.05.2024.

NB: Jisajili na Meridianbet na cheza michezo ya kasino ya mtandaoni upate ushindi kirahisi, Pia ongeza maokoto yako kwa kubashiri michezo mbalimbali yenye ODDS KUBWA. PIGA *149*10# AU tembelea tovuti yao meridianbet.co.tz

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mohamed Nyundo pamoja na Wataalam wengine wamesili katika Mji mdogo wa kilwa kivinje wilaya Kilwa mkoani Lindi kwa usafiri wa boti kutoka Somanga kupitia baharini kwa ajili ya kuangalia hali Miundombinu na kuwafikia Wananchi kutokana na mawasiliano ya Barabara ya Lindi – Dar- es Salaam kukatika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha zilizoambatana na kimbunga Hidaya, leo tarehe 05 Mei 2024.






Na. Dennis Gondwe, KIWANJA CHA NDEGE

WANANCHI wa Mtaa wa Osterbay, Kata ya Kiwanja cha Ndege Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamejitokeza kufanya usafi wa mazingira katika eneo la Shule ya Msingi Mlimwa B kwa lengo la kuweka mazingira safi na kuepuka na magonjwa ya mlipuko kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla.

Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Mtendaji Mtaa wa Osterbay, Ashura Iberia alipokuwa akiongea na wananchi wa Mtaa wa Osterbay waliojitokeza kwa wingi kufanya usafi wa mazingira katika Shule ya Msingi Mlimwa B.

Iberia alisema “leo tumefanya usafi wa mazingira kuzunguka Shule ya Msingi Mlimwa B, wananchi wa Mtaa wa Osterbay wamejitokeza kwa wingi kufanya usafi wa mazingira. 

Lengo la kufanya usafi huo ni kuweka mazingira ya shule safi ili wanafunzi ambao ni watoto wetu wasome katika mazingira safi na salama. Lakini pia kuwaepusha wanafunzi na jamii inayozunguka shule hii na magonjwa ya mlipuko. Zoezi hili nimelisimamia mimi mwenyewe Afisa Mtendaji Mtaa wa Osterbay ili kutoa chachu na hamasa kwa usafi wa mazingira kwa kila mwananchi”.

Kwa upande wake, Kaimu Mwenyekiti wa Mtaa wa Osterbay, Hussein Ngura alisema kuwa kuanzia siku hiyo usafi ni agenda ya mtaa. “Kuanzia leo agenda yetu kuu ya Mtaa wa Ostebay ni usafi wa mazingira kama alivyosema Afisa Mtendaji wa Mtaa. Kama tutakumbuka aliwahi kufika hapa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma na kukagua usafi kwa kustukiza. 

Sasa hatujui ni kiongozi gani atafuata kuja kukagua, hivyo lazima tujipange kwa kuweka mazingira yetu safi. Wananchi wa Mtaa wa Osterbay mmenitendea imani kuwa nina watu kwa jinsi mlivyojitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hili la usafi wa mazingira. Pia, mimi namsifu sana Afisa Mtendaji wa Mtaa wetu kwa kazi nzuri anayofanya, hakika ni mchapa kazi hodari na anatuongoza vizuri” alisema Ngura.

Zoezi la usafi wa mazingira katika Mtaa wa Osterbay, Kata ya Kiwanja cha Ndege liliongozwa na Afisa Mtendaji wa Mtaa, na kuhudhuriwa na wenyeviti, mabalozi na mamia ya wananchi.




Top News