THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

RAIS DKT MAGUFULI AENDESHA MKUTANO WA 11 WA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO


 Mwenyekiti wa Baraza la  Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiwasili kuendesha mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018. Kulia kwake ni   Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Joakim Mhagama na kushoto kwake ni  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel 
 Mwenyekiti wa Baraza la  Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akisalimiana na Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Dkt. Reginald Mengi  alipowasili kuendesha mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018. 
 Mwenyekiti wa Baraza la  Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa meza kuu  na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na walemavu Mhe. Jenista Joakim Mhagama na kushoto kwake ni  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel  na Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Dkt. Reginald Mengi  akijiandaa kufungua  mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018.  
 Sehemu ya Mawaziri, Wabunge na wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI


MJADALA: Ni Yupi Afisa Mawasiliano wa Karne ya 21


MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI UJENZI WA SEKONDARI MICHEWENI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa mkoa wa Kaskazini Pemba kushirikiana katika shughuli za maendeleo. 

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha Afya cha Huduma ya Mama na Mtoto Shumba Vyamboni wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba. 

Kituo hicho cha Mama na Mtoto cha Shumba Vyamboni kitatoa huduma za Mama na Mtoto ambapo jumla ya Wananchi 5,593 wakiwemo wanawake wenye uwezo wa kuzaa 1543 na watoto chini ya umri wa miaka mitano 984 watapata huduma bora ya uzazi, lishe na ustawi wa mama na mtoto. 

Vijiji vitakavyofaidika na huduma ya kituo hicho ni pamoja na Kibubunzi, Kikunguni, Mihogoni, Nyuma ya Mti, Mgeninje, Utaani, Shumba vya Mboni, Uwondwe, Mamoja, Gombe, Uwaani na Bule. 

Katika ziara hiyo yenye lengo la kuhimiza shughuli za maendeleo Makamu wa Rais alikagua ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Micheweni pamoja na kumtembelea Muasisi wa Chama Cha Mapinduzi Bi. Mrashi ambapo alimkabidhi mabati ya kuezekea nyumba yake inayojengwa na wanachama wa chama cha Mapinduzi katika eneo la Sizini. 

Mwisho Makamu wa Rais aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa Tawi la CCM la Ukunjwi ambapo aliwaambia wakina Mama kuwa mstari wa mbele katika kuonesha njia ya kuwa kiongozi bora. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki ujenzi wa skuli ya Sekondari Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mwonekano wa ujenzi wa skuli ya Sekondari Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba


UFAFANUZI WA BASATA KUHUSU KUFUNGIA KAZI ZA SANAA ZILIZOKOSA MAADILI


MWAKILISHI BENKI YA DUNIA AFANYA MAZUNGUMZO NA JAJI MKUU,ARIDHISHWA UTEKELEZAJI MRADI MABORESHO WA HUDUMA ZA KIMAHAKAMA

Na Mary Gwera, Mahakama

Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Miradi ya Utawala Bora kutoka Benki ya Dunia (WB), Bi. Nicola Smithers ameipongeza Mahakama kwa utekelezaji wake wa Mradi wa Maboresho wa huduma za Kimahakama.

Bi. Smithers aliyasema hayo mapema Machi 19, alipokutana na Mhe. Jaji Mkuu ofisini kwake Mahakama ya Rufani-Dar es Salaam ambapo alipata nafasi ya kuongea na Mhe. Jaji Mkuu na Viongozi wengine wa Mahakama akiwemo Mtendaji Mkuu na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania.

“Nimefurahishwa na maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Maboresho ya huduma za Mahakama unaofadhiliwa na Benki ya Dunia, hususani katika eneo la uondoshaji wa mlundikano wa mashauri,” alisema Bi. Smithers

Akimkaribisha ofisini kwake, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahimu Juma alimueleza Bi. Smithers juu ya maboresho mbalimbali yanayoendelea kufanyika ndani ya Mahakama ya Tanzania yote yakiwalenga wananchi ambao ndio wateja wa Mahakama.

“Miongoni mwa maeneo ambayo tunayoendelea kupambana nayo ili kurejesha imani ya wananchi kwa Mahakama ni pamoja na Rushwa, katika hili tmefanya jitihada kadhaa ikiwa ni pamoja na kusambaza mabango ‘posters’ yenye ujumbe wa kupinga rushwa na kuyasambaza katika ofisi za Mahakama kote nchini pamoja na kusambaza simu za kuwawezesha wananchi wenye malalamiko kutuma meseji ili malalamiko yao yaweze kufanyiwa kazi,” alieleza Mhe. Jaji Mkuu.
Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Miradi ya Utawala Bora kutoka Benki ya Dunia (WB), Bi. Nicola Smithers akisaini Kitabu cha Wageni pindi alipowasili ofisini kwa Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mahakama ya Rufani-Dar es Salaam.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahimu Juma akiongea jambo na Mgeni wake Bi. Nicola Smithers ambaye ni Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Miradi ya Utawala Bora kutoka Benki ya Dunia (WB).
Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga (wa pili kushoto) akichangia jambo katika Mazungumzo hayo, wa kwanza kushoto ni Msajili Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revokati, wa pili kulia ni Meneja kutoka Benki ya Dunia-Tanzania, Bw. Dennis Biseko.
Msajili Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revokati (wa kwanza kushoto) akichangia jambo
Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Miradi ya Utawala Bora kutoka Benki ya Dunia (WB), Bi. Nicola Smithers akizungumza jambo.
Mkuu wa Kitengo cha Maboresho-Mahakama, Mhe. Zahra Maruma akiwa katika mazungumzo hayo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


WAIMBAJI MAHIRI WA NYIMBO ZA INJILI KUTIKISA KANDA YA ZIWA TAMASHA LA PASAKA APRILI MOSI


Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
KADIRI kengele inavyogonga kuashiria sikukuu ya Pasaka ipo jirani, ndivyo dhahiri kuwa siku za kuelekea Tamasha la Pasaka zinahesabika. Ni Aprili Mosi, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.
Tumezoea mara nyingi kushuhudia Tamasha la Pasaka likifanyika jijini Dar es Salaam lakini waandaaji wa tamasha hilo wameamua mwaka huu iwe zamu ya Kanda ya Ziwa. Hivyo Pasaka hii, watu wa Kanda ya Ziwa watahemewa kwa burudani ya nyimbo zenye kumsifu na kumtukuza Mungu na litanenwa neno la Mungu.
Hivyo Aprili Mosi ni CCM Kirumba, Aprili Pili Tamasha la Pasaka litachukua nafasi kwenye Uwanja wa Halmashauri, mkoani Simiyu. Hakuna ubishi tena katika sikukuu ya Pasaka mwaka huu wakazi wa Kanda ya Ziwa, eneo ambalo litakuwa sahihi kwao kuisheherekea siku hiyo ni kwenye Tamasha la Pasaka.
Wakati siku zikikaribia kuelekea Tamasha la Pasaka kwa mkazi wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa jumla ni kuendelea kumuomba Mungu ili aendelee kukupa uzima na afya njema.Waandaaji wa tamasha hilo, Kampuni ya Msama Promotion, mwaka huu wameamua kuweka vionjo tofauti ili kuhakikisha tamasha hilo linafanyika na  kuacha historia kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa.
 Kila mwanamuziki aliye kwenye chati, nyimbo zake za kumsifu na kumtukuza Mungu zikiwa zinatamba na kusikika, atakuwemo kuburudisha mashabiki wake.Kwa mujibu wa waandaji wa Tamasha la Pasaka, kati ya wengi watakaofanya kweli, atakuwepo mwanamuziki maarufu nchini Rose Mhando na wengine zaidi ya 15 kutoka ndani na nje ya nchi.Inafahamika kuwa Rose Muhando huwa hahitaji utambulisho. Ni mwanamuziki mwanamuziki mkubwa ambaye Muumba wa Mbingu na Ardhi amemjaalia kipaji cha kuimba kilichoambatana na sauti maridadi. Muziki wa Rose Mhando unapopigwa wapo ambao wanasimamisha shughuli zao kwa muda.
Natamani kutaja baadhi ya nyimbo zake atakazoimba siku hiyo lakini acha nikae kimya. Sitaki kukumalizia uhondo. Vema ufike CCM Kirumba kisha Uwanja wa Halmashauri, Simiyu ili macho na masikio yako yapate kumuona na kumsikiliza Rose Mhando. Uwezo wake wa kuimba umemfanya awe nyota ya muziki wa Injili.Kwa Rose Mhando mwenyewe anajua ukubwa wa Tamasha la Pasaka. 


RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WATENDAJI WAKUU WA KIWANDA CHA BIA TANZANIA BREWERIES LIMITED (TBL) IKULU JIJINI DAR ES SALAAM


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Ricardo Tadeu Rais wa Kampuni ya Anheuser-Busch InBev katika ukanda wa Afrika ambao ni Wanahisa wakuu wa Kampuni ya Bia ya Tanzania Breweries Ltd kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Phillip Mpango kabla ya kuanza kikao chake na Rais wa Kampuni ya Anheuser-Busch InBev Ricardo Tadeu katika ukanda wa Afrika ambao ni Wanahisa wakuu wa Kampuni ya Bia ya Tanzania Breweries Ltd ambayo inatarajia kujenga kiwanda kikubwa cha Bia mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo mara baada ya kikao chake na ujumbe wa Kampuni ya Bia ya Tanzania Breweries Ltd uliokuwa ukiongozwa na Rais wa Kampuni ya Anheuser-Busch InBev Ricardo Tadeu ambao ni wanahisa wakuu wa Kampuni hio ya TBL.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Kampuni ya Anheuser-Busch InBev Ricardo Tadeu mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mmoja wa Wakurugenzi wa TBL katika ukanda wa Afrika Mashariki Roberto Jarrin mara baada ya mazungumzo na ujumbe huo.
Rais wa Kampuni ya Anheuser-Busch InBev Ricardo Tadeu ambao ni wanahisa wakuu wa Kampuni ya TBL akizungumza na wanahabari kuhusu TBL ambayo itajenga kiwanda kikubwa cha Bia mkoani Dodoma.PICHA NA IKULU


MAWAZIRI WA AFYA KUTOKA NCHI 10 WAJADILIANA NAMNA YA KUSHIRIKIANA KATIKA SEKTA AFYA

Na Said Mwishehe,Globu ya Jamii

MAWAZIRI wa Afya kutoka nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini wamekutana nchini Tanzania kwa ajili ya kujadili namna ya kuboresha huduma za afya na hasa katika utambuzi na kubaini magonjwa ya mlipuko.

Pia mawaziri hao wamekutana kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika utoaji na usimamizi bora wa huduma za afya.Mbali ya mawaziri pia wadau wa sekta ya afya kutoka kwenye baadhi ya mashirika wameshiriki mkutano huo.

Kupitia mkutano huo wa afya wa 65 nchi zisizo na uzoefu zitajifunza kutoka nchi ambazo zinafanya vizuri katika utoaji huduma,usimamizi na kutathimi ambapo washiriki wakiwamo mawaziri wa afya pamoja na wadau wa afya wameendelea kubadilisha uzoefu kupitia mada mbalimbali zinazoendelea kutolewa na watoa mada.

Kwa Tanzania, mwenyeji wa mkutano huo ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ni miongoni mwa wanaoshiriki mkutano huo unaojadili masuala ya afya kwa nchi hizo.

Kauli mbiu katika mkutano huo inasema "Ushirikiano wa sekta ya afya katika kupata mafanikio ya malengo ya maendeleo endelevu(SDG's)" na mkutano huo huo utakaofanyika kwa siku tatu inasema hivi.

Hivyo nchi mbalimbali wameelezea namna ambavyo wamekuwa wakikabiliana na changamoto mbalimbali katika sekta ya afya.Mwakilishi kutoka nchi ya Uganda pamoja na kuelezea ambavyo wamefanikiwa katika sekta ya afya lakini changamoto kubwa ipo katika ajali za barabarani ambazo nyingi zinatokana na uendeshaji usifuata sheria unaofanywa na waendesha pikipiki.

Akizungumza kwenye mkutano huo Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema nchini Tanzania kuna mikakati mbalimbali ya kuboresha huduma za afya.Pia ameelezea hivi karibuni watazindua chanjo ya kansa kwa msichana wa kike kuanzia miaka 9 hadi miaka 13.

Amesema lengo ni kukabiliana na tatizo la ugonjwa wa kansa na lengo la Serikali ni kuhakikisha ugonjwa wa kansa unapungua.Wakati wa mkutano huo pia wamejadili sera mbalimbali kwa kila ambazo zipo kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya.


HOTUBA YA RAIS WA TFF ALIPOZUNGUMZA NA WAHARIRI WA HABARI ZA MICHEZO LEO JIJINI DAR

UTEKELEZAJI WA TFF KATIKA MAENEO MBALIMBALI

Ndugu Waandishi wa Habari,Sekretarieti ya TFF, Watanzania wote wanaotuangalia na kutusikiliza,mabibi na mabwana habari za asubuhi.

Naomba nianze kwa kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kukutana mahali hapa siku ya leo tukiwa wazima wa Afya,Lakini pia nichukuwe nafasi hii kuishukuru Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dr.Joseph Pombe Magufuli kwa ushirikiano mkubwa ninaoupata katika uendeshaji wa mpira wa miguu, nimekuwa karibu sana na Serikali kuhakikisha juhudi zetu za kuendeleza mpira zinafanikiwa kwa kasi kubwa sana na mafanikio ya ujio wa Rais wa FIFA ni kielelezo cha karibuni kuonyesha ushirikiano mkubwa tunaoupata toka kwa Serikali hasa Waziri mwenye dhamana ya michezo Mh.Dr,Harrison Mwakyembe na timu yake.

Lakini niwashukuru kwa nafasi ya kipekee ndugu zangu Waandishi wa Habari kwa kazi kubwa mnayoifanya kuhabarisha umma kuhusu habari za mpira wa miguu,Pia pongezi zenu kwa kazi nzuri mliyoifanya wakati wa ujio wa FIFA, mlifanya kazi kubwa sana kutangaza ziara ya Rais wa FIFA, mmetupa heshima kubwa sana.

Ndugu zangu, leo nitaongelea mambo makubwa mawili ili waTanzania wapate kufahamu kinachoendelea katika mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini.Moja nitaongelea kuhusu mambo ambayo tumeyafanya kwa kipindi cha miezi saba nilichokuwepo madarakani lakini la pili ni mambo yanayoendelea sasa hivi kwenye Shirikisho.MKUTANO WA NNE WA BARAZA KUU LA CHAMA CHA ZAPSWU WAFANYIKA ZANZIBAR


 Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wafayakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania TALGWU, Obadia Mwakasitu akizungumza katika Kikao cha Baraza la nne la ZAPSWU huko katika ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi
 Mgeni rasmi wa Kikao cha Baraza kuu la nne la Chama cha Wafayakazi wa Sekta ya Umma, Mw. Khamis Mwinyi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi ZATU akiwahutubia washiriki wa wa Kikao hicho.
 Mwenyekiti wa Chama cha Wafayakazi wa Sekta ya Umma Zanzibar akizungumza machache na kumkaribisha mgeni Rasmi katika kikao cha Baraza kuu la nne la Chama hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi Zanzibar.
 Washirki wa kikao cha Baraza kuu la nne la Chama Wafayakazi wa Sekta ya Umma Zanzibar wakiimba nyimbo maarufu ya Mshikamano katika kikao hicho.
Picha ya pamoja ya Wajumbe walioshiriki kikao cha Baraza kuu la nne la Chama cha Wafayakazi wa Sekta ya Umma Zanzibar ZAPSWU. Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar 


KAIMU MGANGA MFAWIDHI HOSPITALI YA KITETE ASIMAMISHWA KUPISHA UCHUNGUZI WA KITAALAMU

NA TIGANYA VINCENT

19 MACHI 2018

SERIKALI ya Mkoa wa Tabora kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo imeamua kumsimamisha Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Kitete Dkt. Nassoro Kaponta ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zilizotolewa na wananchi dhidi ya Hospitali hiyo.

Maazimio hayo yalitolewa jana mjini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri mara baada ya kikao na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na Wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa Kitete.

Alisema Dkt Kaponta anasimamisha sio kama yeye katenda kosa bali ni katika uwajibikaji ili kupitisha Kamati Maalumu ya Kuchunguza Kitaalamu (Therapeautic Committee) kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wa tuhuma zilizotolewa na wananchi kuhusu mwenendo wa wa Watumishi wa Hospitali hiyo ambaye yeye alikuwa akiisimamia.

Mwanri alitaja baadhi ya tuhuma ni pamoja na lugha chafu kutoka kwa baadhi ya Wauuguzi wanazitoa kwa wakimama wajawazito wanapokwenda kupatiwa huduma ya kujifungua, wagonjwa kudaiwa rushwa na baadhi ya wafanyakazi na vifo wa wakinamama vinavyotokana na uzembe.

Alisema pamoja na Kamati hiyo kuchunguza mambo ya Kitaaluma pia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB) Mkoani Tabora imepewa jukumu la kuchunguza tuhuma zinazotolewa na wananchi wanaoenda kutibiwa pale za rushwa na lugha chafu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


KAMATI YA USTAWI WA JAMII YA BARAZA LA WAWAKILISHI YAFANYA ZIARA KATIKA WIZARA YA AFYA ZANZIBAR.

 Waziri wa Afya wa Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed akiikaribisha Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi ilipofika ofisini kwake Mnazi mmoja kwa ajili ya kutoa mrejesho wa ziara yake iliyofanya katika Vitengo vya Wizara hiyo.
 Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dkt. Mwinyihaji Makame Mwadini akizungumza machache kabla ya Wajumbe wa Kamati yake kuchangia taarifa ya ziara yao kwa Vitengo vya Wizara hiyo.
 Katibu wa Wizara ya Afya, Asha Abdulla akisoma taarifa ya Utekelezaji wa kazi za Wizara kwa kipindi cha mwezi Octoba-Disemba 2017/2018 mbele ya Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi.
 Mjumbe wa Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi, Mwanaasha Khamis Juma (katikati) akichangia taarifa iliyotolewa ya Kamati yao kwa Wizara ya Afya.
 Mjumbe wa Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi, Masoud Ibrahim ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Bububu akipitia taarifa ya Utekelezaji wa kazi za Wizara ya Afya kwa kipindi cha mwezi Octoba-Disemba 2017/2018. Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Wizara ya Afya mnazi mmoja. Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar.


Mhagama: Kilimo cha miwa fursa kwa vijana

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye  Ulemavu  Mhe.Jenista Mhagama amewataka vijana kuchangamkia fursa zilizopo nchini na kuacha kulalamika kuhusu ukosefu wa ajira.
Akizungumza baada ya uzinduzi wa mradi wa shamba darasa kuwezesha wakulima wa nje (outgrowers) wa kiwanda cha Sukari cha Mkulazi  mwishoni mwa wiki katika eneo la Dumila wilayani Kilosa mkoani Morogoro,Waziri Mhagama amesema kundi la vijana linapaswa kuzifuata fursa zilipo na sio kusubiri kuletewa.
Waziri Mhagama amesema serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imejidhatiti kupunguza tatizo la ajira kwa kutekeleza miradi mikubwa ya kitaifa lakini vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa wanapoteza muda mwingi katika mitandao ya kijamii.
“Takwimu zilizopo kwamba 56% ndio nguvu ya vijana,pia 60.7% ya ajira nchini zinapatika kwenye fursa zinazotokana na kilimo lakini vijana hawa hawataki kabisa kusikia habari za kilimo,” amesema Waziri Mhagama.
Waziri Mhagama amebainisha kuwa  serikali inaboresha mazingira ya kilimo kwa kutenga ardhi na mikopo kwa vijana lakini vijana bado wameonekana kutochangamkia fursa hiyo.
“Kujitokeza kwa vijana katika mradi huu ni wito kwa vijana wengine nchini kuelewa kuwa utajiri unapatikana shambani,njooni tutawapa mashamba mlime miwa na Mkulazi watawasaidia kufikia malengo yenu”, amesema waziri huyo huku akiwapongeza kikundi cha vijana wa KCL ambao walikutana katika mtandao wa ‘WhatsApp’ na kuamua kutafuta mashamba kwa ajili ya kilimo cha miwa.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu  Mhe.Jenista Mhagama akipanda miwa ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa shamba darasa kwa wakulima wa nje (Outgrowers) wa Wilaya ya Kilosa . Mpango huo unaratibiwa na kiwanda cha sukari cha Mkulazi kinachomilikiwa na PPF, NSSF pamoja na Jeshi la Magereza na unalenga kuwajengea uwezo wakulima ili kuzalisha miwa yenye ubora na kuiuza kiwandani hapo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye  Ulemavu Jenista Mhagama akisisitiza jambo baada ya kukagua shamba la miwa la kiwanda cha sukari cha Mkulazi-Mbigiro mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki. Wanaomsikiliza kutoka kulia ni Mkurugenzi wa NSSF Profesa Godius Kahyarara na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk.Steven Kebwe.Kushoto ni Mkurugenzi wa PPF Bw.Wiliam Erio. Kiwanda hicho kinachomilikiwa na PPF, NSSF pamoja na Jeshi la Magereza kinatarajiwa kutoa ajira 100,000 na pia kitazalisha tani 250,000 za sukari kwa mwaka.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


KAMATI YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA YATEMBELEA CHANZO CHA MAJI, IFUNDA

Kamati ya Kudumu ya Bunge Biashara na Mazingira mwishoni mwa wiki imetembea chanzo cha Maji ‘Mkaa’ kilichopo Tarafa ya Kiponzelo, Kata ya Ifunda, Mkoani Iringa.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Innocent Bashungwa ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Iringa kwa jitihada zao za kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya kunyweshea mifugo ili kuendelea kulinda vyanzo vya maji na kuwataka kuondoa miti iliyopo pembezoni mwa chanzo hicho ambayo inanyonya maji kwa wingi.

Kwa upande mwingine, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola amezitaka Halmashauri na Wilaya zote nchini kupanda miti kwa wingi ambayo ni rafiki kwa mazingira. “Endapo tutapanda miti kwa wingi, tutaendelea kuwa na mvua za kutosha na kila Halmshauri zinatakiwa kuwa na Sheria ndogo ndogo za Mazingira”.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza amewataka waheshiwa wabunge kuwa mstari wa mbele kuhimiza kilimo cha umwagiliaji kwa kutimia ‘matone’ ili kupunguza matumizi ya maji katika maeneo yao.
Diwani wa Kata ya Ifunda Bw. Elicus Chumila Ngwetta akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira mara baada ya kutembelea eneo la Ifunda na kujionea chanzo cha maji ‘Mkaa’ kilichohifadhiwa vizuri. Uhifadhi wa vyanzo vya maji ni muhimu sana kwa mustakabali wa nchi yetu. Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Kangi Lugola.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Kangi Lugola akifafanua jambo mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira. Kamati ya Bunge mwishoni mwa wiki ilipata fursa ya kutembelea chanzo cha maji ‘Mkaa’ kilichopo Tarafa ya Kiponzelo, Kata ya Ifunda, Mkoa wa Iringa.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Kangi Lugola akisisitiza jambo mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira mara baada ya kutembelea chanzo cha maji ‘Mkaa’ kinachopeleka maji yake Mto Lyandembela ambao nao unamwaga maji Ruaha Mkuu mwaka mzima, Mto ambao ni muhimu sana kwa ustawi wa viumbe hai. Kushoto ni Mhe. Hawa Mwaifunga na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Innocent Bashungwa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza akiwaonyesha waheshimiwa wabunge wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya mifugo kunywa maji katika eneo la Ifunda ikiwa ni jitahada za Mkoa huo kuhifadhi vyanzo vya maji.


Wagonjwa 25 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua katika kambi maalum ya matibabu

Na Mwandishi Maalum

Jumla ya wagonjwa 25 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua katika kambi maalum ya matibabu ya siku sita inayofanyika  katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Upasuaji huo unafanywa na madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya nchini Australia.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi leo jijini Dar es Salaam  Daktari bingwa wa upasuaji wa  moyo na mishipa ya damu ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya upasuaji Bashir Nyangasa alisema wagonjwa watakaofanyiwa upasuaji watoto ni  15 na watu wazima 10.

Dkt. Nyangasa alisema kambi hiyo imeenda  sambamba na upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wagonjwa 65 kati ya hao watoto 35 na watu wazima  30. Wagonjwa ambao wamefanyiwa uchunguzi na hawatafanyiwa upasuaji katika kambi hiyo watafanyiwa upasuaji na madaktari wa JKCI.

“Watoto tunaowafanyiwa upasuaji ni wale wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo ambayo ni matundu na mishipa ya damu kutopitisha damu  vizuri katika moyo na kwa watu wazima tunapandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting) na kubadilisha milango ya moyo miwili hadi mitatu iliyoziba au haifungi vizuri.

Kabla ya kuanza kwa kambi hiyo kulikuwa na mafunzo ya kiuguzi ya siku tano ya utoaji  huduma bora kwa  wagonjwa wa upasuaji wa moyo  yalitolewa na Taasisi ya Open Heart International kwa  wauguzi 30 wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.

Hadi sasa wagonjwa wanne wameshafanyiwa upasuaji wa moyo  kati ya hao watoto wawili na watu wazima wawili na hali zao zinaendelea vizuri.


JWTZ – KUJENGA VIWANDA KATIKA KAMBI ZA JKT

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Salvatory Mabeyo akimuelekeza kitu mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi Christina Mndeme ambaye ameshika punje za mahindi kiganjani kwake, alipotembelea kiwanda cha kisasa cha kuchakata mahindi cha kikosi cha JKT Mlale Songea Mkoani Ruvuma. “ Tunakikosi cha JKT Mbalali kilichopo Mbeya kinalima zao la kahawa na niwazalishaji wazuri wa zao hilo napotutajenga kiwanda cha kuchakata kahawa ili tuwe na Kahawa Product ya JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA ,Tunasambaza viwanda hivi kwa faida ya wananchi wa Tanzania, kwa maendeleo yao ,kwa maendeleo yetu wote, tunaimani tumeanza kuthubutu,tunaimani tutaweza ”


TIGO TANZANIA NA UBER WAUNGANA KULETA OFA MPYA KWA WATEJA WA DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari(wa pili kushoto) akipeana mikono na Meneja Mkuu wa Uber Afrika Mashariki, Loic Amado(wa pili kulia) mara baada ya kuingia makubaliano ya kipekee yatayowafaidisha watumiaji wa Tigo wakaotumia huduma za usafiri za Uber kwa kutumia Uber App bure. Kulia ni Mkurugenzi Mkaazi wa Uber Tanzania, Alfred Msemo na kushoto ni Afisa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Fedha wa Tigo, Hussein Sayed kwenye hafla iliyofanyika jijini Dar Es Salaam jana.

Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo Tanzania imeingia katika makubaliano ya kipekee na kampuni ya kiteknologia ya Uber. Kuanzia leo, wateja wote wa Tigo watatumia huduma za Uber App bure! Makubaliano haya ya aina yake yatawafaidi watumiaji wa huduma za usafiri za Uber pamoja na madereva waliojiunga na mfumo huo. 


“Tigo ni nembo pana ya biashara katika soko la Tanzania na tuna wajibu wa kuzindua njia bora zaidi kwa wateja kujumuika katika maisha yanayowazingira. Makubaliano haya na Uber yanaboresha bidhaa na huduma ambazo wateja wetu wanafurahia katika maisha yao ya kila siku,” Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari alisema. 
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari (kushoto) akizungumza katika hafla ya kuingia makubaliano ya kipekee yatayowafaidisha watumiaji wa Tigo wakaotumia huduma za usafiri za Uber kwa kutumia Uber App bure, iliyofanyika jijini Dar Es Salaam leo. Wengine pichani kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkaazi wa Uber Tanzania, Alfred Msemo, Meneja Mkuu wa Uber Afrika Mashariki, Loic Amado pamoja na Afisa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Fedha wa Tigo, Hussein Sayed.

Naye Alfred Msemo, Mkurugenzi wa Uber alisema, “Tunafurahia makubaliano haya na Tigo yatakayowawezesha watumiaji na madereva wa huduma za Uber waliojisajili na mtandao wa Tigo kutumia huduma ya Uber App bure kwenye simu zao za mkononi bila tozo lolote la gharama za data. 

Uber ni mfumo wa simu za kisasa unaowezesha watu kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa kubonyeza kitufe tu! Lengo kuu la Uber ni kuwezesha usafiri salama, wa uhakika na kwa gharama nafuu kwa kila mtu, kila sehemu. Makubaliano haya yatawahamasisha maelfu ya wakaazi wa Dar es Salaam ambao wamejisajili na mtandao wa Tigo kutumia Uber App kwa ajili ya huduma za usafiri jijini Dar es Salaam,’ Msemo alibainisha. 
Kampuni hizi mbili zitashirikiana katika bidhaa na promosheni zitakazoboresha huduma kwa wateja wa sasa na wa siku zijazo. Tigo na Uber nchini Tanzania wanatarajia kutangaza ofa zaidi kabambe zitakazowawezesha wateja kufurahia huduma za Uber jijini Dar es Salaam ambapo huduma za Uber zinapatikana kwa sasa. 


ATAKAYEHUJUMU UJENZI WA MRADI WA MAJI TOKA ZIWA VICTORIA KUKIONA - RC MWANRI

SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imesema itamchukulia hatua kali mtu yoyote atakayebainika kuhujumu utekelezaji wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Mkoani humo wenye gharama ya bilioni 600 kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa eneo hilo.

Kauli hiyo imetolewa leo wilayani Nzega na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wakati alipotembelea na kukagua mradi huo unaotoa maji katika Kijiji cha Solwa mkoani Shinyanga kupeleka mkoani Tabora ambapo wilaya za Nzega, Igunga, Uyui na Tabora mjini zitanufaika na mradi huo wa maji kutoka ziwa Victoria unaotekelezwa kwa muda wa miezi thelathini.

Alisema kuwa Serikali haitamfumbia macho mtu yeyote atakayebainika kuwa na nia ovu ya kutaka kuiba vifaa mbalimbali ambavyo vinatumiwa na wakandarasi katika kujenga mradi huo ambao ni muhimu sana kwa ajili ya wakazi wa maeneo mbali ya Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akizungumza na Mkandarasi na wananchi baada ya kutembelea na kukagua mradi wa maji kutoka ziwa Victoria jana ambapo mradi huo unaotoa maji katika Kijiji cha Solwa mkoani Shinyanga kupeleka mkoani Tabora ambapo wilaya za Nzega,Igunga,Uyui na Tabora mjini zitanufaika na mradi huo wa maji kutoka ziwa Victoria unaotekelezwa kwa muda wa miezi thelathini. 

Mwanri alisema kuwa hadi sasa kazi inaendelea ambapo Mkandarasi ya kampuni ya L & T yupo kazini akiendelea na shughuli ya kuunga na kufukia mabomba ardhini na kueleza kuwa hujuma yoyote ambayo inaweza kujitokeza inaaweza kusababisha mradi kuchelewa kumalizika kusababisha wakazi wa maeneo ambao yalikuwa yapate huduma hiyo kuendelea kupata matatizo ya maji.

Alisema kuwa kama kuna matatizo yoyote wanayopata kama vile wizi wa vifaa ni vema wakaeleza ili uongozi wa Mkoa uweze kuchukua hatua mapema kwa ajili ya kuendelea kuwawekea mazingira mazuri ya ujenzi wa mradi huo na kuongeza kuwa kama watapata matatizo na kunyamaza na muda wa kukamilisha mradi utafika wakiwa bado hawajakamilisha Serikali haitasikiliza.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari baada ya kuungana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora (hayupo pichani) kutembelea na kukagua mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria jana ambapo mradi huo unaotoa maji katika Kijiji cha Solwa mkoani Shinyanga kupeleka mkoani Tabora ambapo wilaya za Nzega,Igunga,Uyui na Tabora mjini zitanufaika na mradi huo wa maji kutoka ziwa Victoria unaotekelezwa kwa muda wa miezi thelathini.

Mwanri aliwataka Wakuu wote wa Wilaya na Watendaji wote ambapo mradi huo unapita kuhakikisha wanasimamia ili isije ikatokee hujuma yoyote na kama ilitokea wakamate watu wote wanatuhumiwa.

Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Mkama Bwire alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo upo ndani ya utekelezaji na tayari hata malipo ya fidia kwa wananchi  waliopitiwa maeneo yao na mradi yamekwishafanyika. Alisema wananchi 204 ambao maeneo yanapitiwa na Mradi huo na kukabainika kuwa wanatarajiwa kulipwa milioni 890.5 zitatumika  kama fidia  kwa wananchi hao

Alisema kuwa jumla ya milioni 760 zimeshalipwa kwa wananchi zaidi ya 162 ambao maeneo yao yalikwishafanyiwa tathmini.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Nzega alisema wananchi wa wilaya yake wanaupokea Mradi huo kwa furaha kwa kukamilika kwake kutasaidia kuwaondolea tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama ya uhakika. Mradi huu wa Maji unatarajia kuwanufaisha wakazi wa Mkoa wa Tabora wapatao milioni moja ambao watakuwa na uhakika wa maji safi na salama.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na Taka Manispaa ya Tabora (TUWASA) Mkama Bwire akitoa ufafanuzi juu ya ulipaji fidia wakati utekelezaji wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria jana mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri kutembelea na kukagua mradi huo.
Baadhi ya Mafundi wa Kampuni ya L & T wakiwa kazini wakiendelea na shughuli ya kuunga na kufukia mabomba ardhini kwa ajili ya kupeleka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Tabora.