Na Mathias Canal, Kaskazini Pemba

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Umeipongeza serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi Visiwani Pemba.

UVCCM imesema kuwa RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amefanya mabadiliko makubwa ya kimaendeleo ikiwemo kuundwa kwa Mamlaka ya Viwanja vya ndege vya Zanzibar jambo ambalo litaongeza mapato kwa serikali na vipato kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka leo Agosti 17, 2017 alipokuwa akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake katika mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa Jamhuri Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akizungumza na kikundi cha wajasiliamali kikundi cha ushoni Mchanga mdogo Mkoa wa Kaskazini pemba wilaya Wete.
Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka(wa kwanza kushoto) akishiriki ujenzi wa Jengo la maskani Mtambwe Wilayani wete.
Wanachama na Viongozi wa CCM na Jumuiya zake Wilaya ya Wete wakifuatilia kwa Umakini mkutano huo.
Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akizungumza katika Mkutano wa ndani akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake katika mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa Jamhuri Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...